Mabadiliko ya cabinet yataondoa uozo huu uliokithiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko ya cabinet yataondoa uozo huu uliokithiri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by heros, Apr 28, 2012.

 1. h

  heros Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina mashaka sana na mabadiliko yanayokusudiwa ya baraza la mawaziri, je yataondoa uozo huu uliokithiri ndani ya serikali ya JK?
   
 2. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wabunge wengi wa ccm washakuwa used ama second hand na hawana jipya kwa nchi hii tena
   
 3. M

  Mkira JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ila tuache kudanyangya badala ya kulibebesha zigo taifa kwa kuchagua waziri Mku mwingine ninamshauri amurudishe Lowassa bila kujali kelele za wapinzani wengineo na familia yake eti Lowassa anataka kumngóa akimurisha hakika Lowassa atachapa kazi na aipaisha CCM, kwa vile Bunge sehemu kubwa ni la CCM Nina imani watamkubali Lowassa na EL hatafanya kosa atalekebisha mengi including shule za kata kero za maji umeme nk!

  HUO NDIO UKWELI KWA SASA JK TUMIA RUNGU LAKO LA KATIBA TEUA TENA LOWASSA UTAFURAHI! NI KATIKA IMANI KUWA HATARUDIA MAKOSA NA WIZI WAKE TENA!!! ILA SIFA YA USIMAMIZI UTARUDISHA UHAI WA CCM , NI MAONI YANGU TU!
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  jk alitakiwa tu akubali nchi imemshinda na astaafu kabla ya muda wake ili kulinusuru taifa. Hii ndo hasara ya kujaza mahawara,watwasi na wapuuzi wengine kwenye mambo yanayohitaji utendaji. Ndo maana hata jamaa wa tra wanaaim padogo na fedha zingine zinaishia mifukoni mwao. Hii ni baada ya kuona fedha zinazokusanywa kwa ajili ya shughuli za maendele zinahamishiwa kwenye mifuko ya familia za wachache. Haiwezekani kama kiongozi wa nchi unakubali mawaziri waishi hotelini na wanalipiwa kodi na wavuja jasho. Wamejengewa nyumba hawataki kuishi sasa wanataka nini kama sio kutudhulumu wananchi tusipate huduma za jamii? Huwa najiuliza siku zote lengo la jk kugombania urais wa nchi hii lilikuwa nn? Bora tungekttwa na utawala wa kifalme ieleweke kwamba kuna watu wamejimilikisha mali za nchi milele yote.
   
 5. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  heros,

  Ukweli ni kwamba hii haitaondoa kabisa uozo uliokithiri ndani ya CCM lakini itapunguza kwa sehemu hii kasi ya utafunaji wa pesa zetu angalao kwa asilimia chache! Huu uoza UTAKWISHA TU PALE SERIKALI YA CCM NA MAGAMBA YAO WATAKAPO ONDOKA IKULU mwaka 2015.

  Kama ulimsikia Mhe. Freeman Mbowe kwenye kikao cha Bunge kilichoisha juzi wakti anachangia hoja za Kamati za Bunge kuhusu utafunwaji wa Pesa za walipa Kodi na ripoti ya CAG alisema KUNA HAJA YA KUBADILISHA THE WHOLE MECHANISM YA UTAWALA KWA MAWAZIRI! Alisema wamepewa madaraka makubwa mno na hivyo wana mamlaka makubwa ya kufanya wanachotaka kuhusu pesa za Serikali wanazopewa kwenye Bajeti za Wizara zao.

  Mimi niliafikiana naye. Kwa stage tuliyofikia kwa sasa hakika ipo haja ya kutazama muundo wa serikali katika Mawizara yetu.
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Never,sana sana watatia tia maji kusubiri kifo cha magamba mwaka 2015.
   
 7. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu kipya hapo Yaani badaala ya Balozi zetu na wizara zetu kuangalia ni jinsi gani zitashiriki katika kuinua uchumi wa nchi yetu katika nyanja mbali mbali hususani ya biashara ya kimataifa kwenye wizara ya mambo ya nje wamejaa usalama wa taifa na kazi yao kubwa ni political diplomacy na siyo economical diplomacy!Kazi ni kupoekea viongozi mbali mbali kutoka nchi za wenzetu na kuratatibu safari za raisi! ebu waangalie kwamfano Wizara ya mambo ya nje na biashara ya nchi kama China,Sweden na Malaysia zimekuwastructured vipi na impact yake nini!Mwisho wa siku mawaziri wetu wanaishi kufanya kazi za kupokea maraisi au wageni mbali mbali na kuzindua miradi.
  PHOTO3 (1).JPG PHOTO4 (1).JPG 5828783337_dc637676a8.jpg
   
Loading...