Mabadiliko makubwa katika siasa za Tanzania

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,486
3,407
Wadau,

Tathmini ya siasa za Tanzania ni kuwa zimeingia katika hatua mpya (the new political trending). Wanasayansi ya siasa wanabainisha kuwa utabiri wa Mwl. Nyerere umetimia. Siasa za nchi kwa sasa zinachagizwa na kuongozwa kwa kuzingatia mielekeo ya mahasimu wawili (political protagonists) – Rais John Pombe Magufuli (JPM) na Ndugu Edward Ngoyaye Lowasa (ENL) – wote makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

JPM anaongoza mrengo wa CCM contemporary revolutionary wakati ENL anaongoza mrengo wa CCM asili. Upinzani ukiwasilishwa na Chadema/Ukawa unatoa makaazi ya muda (temporary shelter) kwa kundi la CCM asili (irony) wakati CCM inatoa mkaazi ya muda kwa kundi la CCM contemporary revolutionary.

Ndani ya kila temporary shelter kuna wakmbizi/wahamiaji wa kisiasa ambao wataondoka muda wowote mara baada ya kunyoosha mambo yao, Haya ni makundi yenye hofu yanayoishi mafichoni ndani ya kundi hasimu.

Katika kundi la CCM contemporary revolutionary kuna akina Chenge, Kikwete na masalia wake ambalo haliridhishwi na namna JPM anakoelekea lakini wamewishapoteza uwezo wa kumzuia na kumdhibiti. Hivyo mkakati wao wa muda mrefu ni kuondoka (permanent exit) kuelekea katika kundi la CCM asili kumfuata ENL akiwa na wakongwe wengine – Kingunge Ngombare Mwiru, Mgeja, Guninita, Msindai na kadhalika.

Ndani ya kundi la Ukawa/Chadema kuna akina Lissu, Waitara, Mnyika , Slaa (amekwishatangulia) na wengineo ambao wataondoka kuelekea kundi la CCM contemporary revolutionary kwa sababu watakuwa wameshindwa udhibiti wa Ukawa/Chadema kutokana na ujio wa kundi kubwa la CCM asili.

Mabadaliko haya tunayoweza kuita Tanzania’s great political trek yanatarajiwa kutokea/kukamilika kati ya sasa na miaka 3 ijayo. Ni wakati huo upinzani rasmi na wenye nguvu hapa nchini utakuwa umenyumbuka na kuzaliwa upya sawia na maono ya Mwl. Nyerere. Hicho ndio kilichotokea Kenya na hata Zimbabwe. Wafuasi/wanachama wa vyama/makundi haya walio wengi watabaki wameduwaa kwa kuwa hawataweza kuelewa kwa haraka na kuamini kitakachokuwa kikitokea mbele ya macho yao. Wanatakiwa kuaza sasa kujiandaa ki-saikolojia. Tusubiri.
 
ndio yale ya joni kutulia kwa saaasa na edo kuibuka kwa kasi .naomba kitwanga 1 baridi hapa kuna utamu............
 
Ulipotaja jina la ENL, Kingunge, Mgeja na wengine kama sehemu ya watu wanaowakilisha kundi la CCM asili, andiko lako zima limekosa mantiki. Kwa kukusaidia tu, rudi kasome kuelewa historia, msingi, kanuni na imani ya chama cha TANU na baadae CCM kwanza kabla hujaja na kutuelea Lowassa anawakilisha kundi la CCM asili.
 
Sophist umeandika kitu ambacho kinafikirisha sana. Siasa zetu hazijitengenezi zenyewe bali zinatengenezwa kulingana na upepo ulivyo.
 
Back
Top Bottom