Mabadiliko Katiba ya CCM -Dola limechukua chama

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,781
3,210
Mabadiliko ya katiba ya CCM yaliyofanyika yamesababisha dola kukisimamia CCM badala ya CCM kuisimamia serikali yake yenyewe , hii ni kutokana na idadi ya wajumbe wa Kamati kuu ya CCM kuwa 24 na kati ya hao 24 wajumbe 15 wanaingia kwa vyeo vyao vya kiserikali ama kwa kuteuliwa na Rais /Mwenyekiti wa CCM .

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ni kama ifuatavyo;


i. Viongozi wakuu wa serikali kutoka bara wako 4 ( Rais,Makamu wa Rais,Spika wa Bunge,Waziri Mkuu

ii. Viongozi wakuu kutoka Zanzibar 3 (Rais , Makamo wa pili wa Rais na Spika wa Baraza

iii. Viongozi wa kuteuliwa na M.kiti CCM 4 (Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti, Naibu Katibu Mkuu Bara , Naibu Katibu Mkuu Zanzibar )

iv. Makatibu wa Halimashauri kuu 4 wanaoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM (Uenezi,Organization,Fedha na Mambo ya nje )

v. Aidha wenyeviti wa Jumuiya 3 wanaingia kwa influence ya Mwenyekiti wa CCM

vi.Hivyo ni wajumbe 6 tu ambao unaweza kuwaita ni wawakilishi wa CCM ambao wanachaguliwa na wanaCCM kwenye vikao ……

Kwa uchambuzi huuwa 4D ,inahitaji akili kubwa kuujadili na sio akili za Kibashite

Sasa ni rasmi kuwa dola limekamata Chama , linakisimamia chama , linakielekeza Chama .......tutashuhudia mengi katika zama hizi.
 
Back
Top Bottom