Maaskofu na Wachungaji zaidi ya 1200 wa Kanisa la Askofu Gwajima watinga Mahakamani Dodoma

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Maaskofu na Wachungaji wanaohudumu kupitia Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church(Ufufuo na Uzima) 'kanisa la Gwajima' wakiingia na kukaa katika chumba cha mahakama hapa katika Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dodoma kwa ajili ya kufuatilia shauri la kanisa wanalohudumu ambalo limezuiwa kutoa huduma kuanzia juni 02, 2025.

Pia, Soma: Kesi ya Kanisa la Gwajima kufungiwa kunguruma leo Dodoma

Viongozi hawa wametoka maeneo mbalimbali nchini na kuja hapa Dodoma ili kujua hatma ya kanisa hilo lililopo chini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo inalenga kulinda hadhi ya usajili wa kanisa hilo huku rufaa dhidi ya zuio hilo ikiendelea kusikilizwa. Kanisa hilo linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM.

Hivi karibuni, mamlaka za Serikali zilifunga kanisa hilo kwa madai kwamba linaendesha shughuli kinyume na masharti ya leseni ya usajili wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka, baadhi ya shughuli zinazofanyika ndani ya kanisa hilo zimeelezwa kuwa ni za ‘kisasa kupita kiasi’, na hazilingani na malengo ya asili ya taasisi hiyo kama ilivyosajiliwa.

Kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala, kanisa hilo limewasilisha shauri namba 13189 la mwaka 2025 dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Msajili wa Taasisi za Kiraia.

Katika shauri hilo, Glory of Christ Tanzania Church inaiomba mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.

Maaskofu na Wachungaji wanaohudumu kupitia Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church(Ufufuo na Uzima) 'kanisa la Gwajima' wakiingia na kukaa katika chumba cha mahakama hapa katika Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dodoma kwa ajili ya kufuatilia shauri la kanisa wanalohudumu ambalo limezuiwa kutoa huduma kuanzia juni 02, 2025.

Viongozi hawa wametoka maeneo mbalimbali nchini na kuja hapa Dodoma ili kujua hatma ya kanisa hilo lililopo chini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.
Hakuna mapandikizi kweli humo?
 
Hakuna Utawala wowote ule hapa duniani ambao umewahi kushinda Vita ya kidini, hakuna!
 
Maaskofu na Wachungaji wanaohudumu kupitia Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church(Ufufuo na Uzima) 'kanisa la Gwajima' wakiingia na kukaa katika chumba cha mahakama hapa katika Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dodoma kwa ajili ya kufuatilia shauri la kanisa wanalohudumu ambalo limezuiwa kutoa huduma kuanzia juni 02, 2025.

Viongozi hawa wametoka maeneo mbalimbali nchini na kuja hapa Dodoma ili kujua hatma ya kanisa hilo lililopo chini yani jambo Askofu Dkt. Josephat Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.
Sawa
 
Aliyetoa uamuzi wa kufungia kanisa kwasababu mtu mmoja ametoa kauli gani sijui ni zaidi ya MPUMBAVU! Yaani wanaiabisha serikali hawa watu. Unakosaje akili kiasi hicho?
Huelewi kitu
Taasisi za din haziruhusiwii kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
 
Hakufunga kwa ajili ya mtu awe Gwajima au Askofu Mwanamapinduzi au yeyote

Kafunga sababu taasisi imeamua kutumia taasisi yao kuwa kichaka cha kuendeshea siasa kinyume na masharti ya usajili wao

Hao wote sijui askofu Gwajima au Mwanamapinduzi au yeyote hawasomeki kwenye hati ya Usajili linasomeka jina la Kanisa tu

Ndio maana msajili kafunga kanisa hawajamfunga Gwajima au Mwanamapinduzi
 
Huelewi kitu
Taasisi za diningazitakiwi kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
Usifikiri kwamba Watu wote kabisa waliopo hapa ni Wajinga au hawana akili Kama ulivyo wewe. Kwa hiyo unataka kusema kwamba Baba wa familia akitenda kosa na kushitakiwa Mahakamani na kisha akakutwa na hatia, basi na watoto wake wote kabisa waliopo kwenye familia hiyo nao watakuwa wametiwa hatiani na kufungwa jela gerezani eti kwa sababu baba yao amefanya makosa??
Au unamaanisha Nini hasa kusema hivyo?
 
Aliyetoa uamuzi wa kufungia kanisa kwasababu mtu mmoja ametoa kauli gani sijui ni zaidi ya MPUMBAVU! Yaani wanaiabisha serikali hawa watu. Unakosaje akili kiasi hicho?
Too bad huwa wanafichwa ili wasionyooshewe vidole ila hao watu ni viongoz wakubwa, kulurupuka si mara ya kwanza , mara kibao wameonyesha kutokufaham wanacho kifanya

Baadae aibu azibebe dpp
 
Usifikiri kwamba Watu wote kabisa waliopo hapa ni Wajinga Kama ulivyo wewe. Kwa hiyo unataka kusema kwamba Baba wa familia akitenda kosa na kushitakiwa Mahakamani na kisha akakutwa na hatia, basi na watoto wake wote kabisa waliopo kwenye familia hiyo nao watakuwa wametiwa hatiani na kufungwa jela gerezani eti kwa sababu baba yao amefanya makosa??
Au unamaanisha Nini hasa kusema hivyo?
Ndio maana huko Ulaya na Binadamu waliostaarabika wanaweza kumsamehe Kosa Mharifu kwa sababu tu ana watu wengine nyuma yake wanaomtegemea ambao wanaweza kuathirika zaidi kwa kufungwa kwake. Huu ni Ustaarabu wa kibinadamu

Kipi bora kumfanga mtu mmoja na kuleta madhara kwa watu 200 au kumwacha na kunufaisha watu 200? Mwafrika ataona bora afjngwe tu ili akome.....hahahaha
 
Huelewi kitu
Taasisi za din haxiruhusiwii kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
NO REFORMS, NO ELECTION
 
Usifikiri kwamba Watu wote kabisa waliopo hapa ni Wajinga au hawana akili Kama ulivyo wewe. Kwa hiyo unataka kusema kwamba Baba wa familia akitenda kosa na kushitakiwa Mahakamani na kisha akakutwa na hatia, basi na watoto wake wote kabisa waliopo kwenye familia hiyo nao watakuwa wametiwa hatiani na kufungwa jela gerezani eti kwa sababu baba yao amefanya makosa??
Au unamaanisha Nini hasa kusema hivyo?
Familia haisajiwi kwa msajili baba wala watoto

Msajili mkataba wa usajili wa taasisi hiyo ni kati yake na taasisi sio kati yake na Gwajima au Mwanamapinduzi au yeyote au mke au mtoto au muumini wa hilo kanisa

Viongozi waliopo na waumini waliopo waweza ondoka hata leo msajili atabaki kuangalia taasisi kama inazingatia maadili na masharti ya usajili tu si vinginevyo

Msajili kafunga sababu ya taasisi kukiuka masharti ya usajili.Hapo hahangaiki na hayo mavazi ya kiaskofu na kichungaji mliyoingia nayo mahakamani hayo hayamtishi msajili wala hakimu ni sheria tu
 
Kwa hiyo akiibuka Mtu leo hii akaenda pale katika Uwanja wa Soka wa Benjamin William Mkapa kisha akaitukana na kuikashifu Serikali, Je, watakaokamatwa na kushitakiwa kwa Kitendo hicho Cha kuikashifu Serikali watakuwa ni Wamiliki wa Uwanja huo wa soka au atakamatwa Mtu binafsi aliyehusika katika kuikashifu Serikali?????
 
Kwa hiyo akiibuka Mtu leo hii akaenda pale katika Uwanja wa Soka wa Benjamin William Mkapa kisha akaitukana na kuikashifu Serikali basi watakaokamatwa na kushitakiwa kwa Kitendo hicho Cha kuikashifu Serikali watakuwa ni Wamiliki wa Uwanja huo wa soka au atakamatwa Mtu binafsi aliyehusika katika kuikashifu Serikali?????
Gwajima hajaibuka tu ni kiongozi wa hiyo taasisi iliyofungiwa na msemaji mkuu wa hiyo taasisi

Mfano wako sio halisia
 
Huelewi kitu
Taasisi za din haziruhusiwii kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
Wewe ndo umehusika kufungia kwa kutumia akili ndogo

Kosa la mchungaji mmoja haliwezi kusababisha watu zaidi ya milioni wawe kwenye kosa hilo hilo

Kamata Gwajima weka ndani, kanisa liendelee

Sielewi nyinyi ccm ni hadi zipite karine ngapi ndio mpate walau akili kidooogo kabisa
 
Kwa hiyo akiibuka Mtu leo hii akaenda pale katika Uwanja wa Soka wa Benjamin William Mkapa kisha akaitukana na kuikashifu Serikali, Je, watakaokamatwa na kushitakiwa kwa Kitendo hicho Cha kuikashifu Serikali watakuwa ni Wamiliki wa Uwanja huo wa soka au atakamatwa Mtu binafsi aliyehusika katika kuikashifu Serikali?????
Uongozi wa uwanja au soko utamkamata na kumkabidhi polisi chap chap

Uongozi wa hilo Kanisa walipaswa wamkamate Gwajima na kumkabidhi polisi na wao wenyewe wamfungulie mashtaka ya kukiuka masharti ya usajili kama wanaona kweli kuwa kazuka tu kwenye kanisa lao

Walikaa kimya hadi kanisa kufungwa siasa chafu zikiendelea ndani ya taasisi
 
Back
Top Bottom