yoga
JF-Expert Member
- Jan 6, 2013
- 1,830
- 8,631
Ni jambo gumu sana kuwafanya watu wa kuelewe pale unapokuwa upo kwenye matatizo, upo kwenye msukumo wa kutafuta suluhu ya matatizo yako, ndani yake ukiwa na suluhu ila una aibu ya utekelezaji wa suluhu hiyo ambayo ninafuu na rahisi kwenye utatuzi wa changamoto hiyo kwa kufikiria watu watakuchukuliaje, siku zote tunajikuta tukifanya maamuzi kwa kufuata watu wanataka uishije na sio wewe kuishi kama wewe, tumekuwa tukihisahau taswira yetu, tukisahau matamanio yetu ya kibailogojia na kiuchumi na kujikuta tukiishi kwa kuridhisha matamanio ya wengine huku tukizidi kuumia kiuchumi na kuwa na msongo wa mawazo ambao hupelekea kuwa na afya migogogro na kukata tama ya maisha.
Tumekuwa na mfumo wa maisha ya kimashindano usio zingatia vipato vyetu na uwezo wetu. Usishangae mtu akawa hana uwezo wa kumiliki gari la kutembelea lakini anakopa na kununua gari, yote sababu flani analo gari na kwasababu hataki kushindwa na mtu huyo basi analinunua kwa mkopo na mwisho wa siku anagundua kuna mafuta, service za mara kwa mara wakati kipato chake hakijitoshelezi hivyo kujikuta katika msongo mkubwa wa mawazo. Mfumo huu wa maisha ni mfumo feki, mfumo usio halisia na wewe bali mfumo wa kutengenezwa na wewe, mfumo huu muonekano wako wanje ni tofauti na muonekano wako wa ndani. Hii inamlazimisha mtu kujiingiza katika mikopo mingiiiiiii ili kutimiza mfumo wake huu wanje.
Mara nyingi huwa tunawaza kufanya mambo makubwa sana lakini uwezo wa kuyafanya ni mdogo kupita maelezo. Hii nikutokana na aina ya maisha tuliyokuzwa nayo kuathiri mfumo wetu wa kiakili kutumia fursa mbalimbali kutatua changamoto tulizonazo. Sisi kama binadamu haswa vijana tunakua katika msongo na mapitio ya vitu vyaaina nyingi sana, tunashawishika na ufikiriaji na mfumo wa maisha ya watu wenye mafanikio na maendeleo kupitia utandawazi na kutamani kuwa kama wao wakati mfumo wa maisha yao, tamaduni zao nitofauti na hizi za kwetu tulio katika bara hili la giza. Ni ukweli usio fichika vijana wengi wa kiafrika tumekua na tamaa ya kuishi maisha mzuri.
Ninapo sema maisha mazuri na maana ya vitu vingi kidogo. Na maana ya mtazamo wa vijana wa kitanzania/Afrika kuhusu dhana ya maisha mazuri. Wengi tunaamini maisha mazuri ni kuwa na Gari nzuri ya gharama, mwanamke/mwanamume mzuri, nyumba nzuri lakini pia kuwa na nguo kalikali za kubadilisha mara kwa mara. Kwa ufupi ni maisha ambayo ni recognizable kwa kila mmoja kwamba ukipita mahala au sehemu Fulani watu wakuone wakujue kuwa ni wewe umepita. Suprising hakuna ajuaye kuwa si dhambi kuwa na maisha ya aina iyo, ila inachukua muda, juhudi, kujituma, kuvumilia, ubunifu na kujitoa kuyafikia maisha ya aina hiyo, ila sasa vijana wengi hatutaki kuvumilia, kujituma kuwa wabunifu na kujituma tunataka shotcuts.
Wengi wenye mtazamo wa shortcut ya maisha ni vijana kuanzia miaka 18 – 35, huu ni umri ambao kwa mfumo wa kimaisha ya afrika unamfanya kijana kuwa na tama ya kutaka maisha mazuri bila kuyaangaikia. Kunamsemo unasema mambo mazuri hayataki haraka lakini kwetu sisi vijana tulio wengi tunaamini mambo mazuri yanataka haraka na dio maana wengi ujikuta wakitafuta shortcuts za kujipatia kipato kikubwa ili wafanikiwe kwa haraka. Mwisho wa siku tunapata wauza unga, mashoga, majambazi, matapeli, madada poa, mamario na wengineo wengi.
Katika uwanja huu wa mchafuko wa kimaisha, vijana ama kijana anapaswa kujitambua nakuwa na moyo wa kushinda tamaaa na vishawishi bila kupoteza lengo la kuwa na mafanikio makubwa. Hii inamaana kama kijana unapaswa kuwa na vipaombele kwenye maisha yako. Lakini unapaswa kuwa na mahitaji kulingana na kipato chako, unapaswa kuwa na maisha ya kushindana kujua kupata mafanikio na sio kununua na kumiliki vitu. Unapaswa kujua kunakukosea na kujifunza kutokea kwenye kukosea kutokurudia makosa na kuyatumia hayo makosa kama solution yakujenga fursa mpya ama kuiendeleza uliyokuwanayo. Kijana unapaswa kutokukata tamaaa, na kufikiri kwa ubunifu, kuweka lengo na malengo kila mwaka, mwezi na wiki.
Unapaswa kuishi kwa budget, kutokuwa na matumizi kupita kipato chako, matumizi yako ya zingatie kipato chako na upate fedha ya kuserve kila unapo pata fedha, jaribu kutambua vile uvipendavyo sanaaa na kama vinakutesa kiuchumi jenga tabia ya kuanza kupunguza na mwisho kuachana navyo kabisa. Kumbuka kuwekeza kwenye vitu productive vitakavyo kupa income kujazia kwenye pato lako.
Kuna kipindi inafika mahala mambo huwa yanakuwa magumu, mfano umeajiriwa mshahara uupatao ni mdogo kwa maana mahitaji yako na ukipatacho kimekua kidogo, mfano kodi ya nyumba imepanda, lakini bado unahitajika kulipa umeme, ulipie maji, mavazi na chakula lakini pia unayo familia inayokutegemea kwa namna moja ama nyingine inafika mahala unapata msongo mkubwa wa mawazo, na ukizingatia una mkopo/ mikopo, haujajenga hauna kiwanja na wapo wenzio kama wewe unawaona wanamafanikio na wanasonga mbele inafika mahala unakata tamaa,unakosa mwelekeo na hapa wengine huwaza pombe kama msaada wa kupunguza mawazo wengine huporomoka kiafya na wengine hufariki ama kukata tamaaa kabisa ya kimaisha.
Kama uko katika hali hii ama unaelekea kuwa katika hali hii, tambua kuwa hauko peke yako, lakini kutokuwa peke yako sio sababu ya wewe kuendelea kuishi maisha hayo. Angalia kipato ulichobakiza kisha angalia ni kwa namna gani unaweza kupunguza matumizi kwa muda kujijenga ili kuwa na maisha mazuri zaidi. Yaani fikiria shida kwa siku kumi ili uishi kwa furaha siku 100. Ondoa aibu kwani hayo ni maisha yako wewe. Tambua ulikuja duniani wewe na unayatengeneza maisha yako wewe na kizazi chako kwa kuwa na chaguzi za njia sahihi za kupita kufikia malengo yako. Una haja ya kushindana kuwa na umiliki wa vitu bali unapaswa kushindana kuwa na njia nyingi zinazo kupa umiliki wa vitu. Sikuzote jifunze namna ya kuendelea na sio kuendelea.
Darasa litaendelea: by madam Yoga