Maandamano 'Yaliyomtikisa' Kagame!

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Bado nikiwa katika viyunga vya hili jiji la Kigali, nimeona si mbaya nikishea nanyi hii stori niliyoipata huku.
Nadhani Meddie Kagere si jina geni nchini Tanzania.
Huyu jamaa alizaliwa katika mji wa Entebe uliopo nchini Uganda. Meddie Kagere alianza kusakata soka katika timu ya Mbale Heroes iliyopo Uganda kabla ya kuhamia nchini Rwanda, ambapo alicheza katika timu kadhaa kabla ya kutua katika miamba ya soka nchini humo, Rayon Sports ambapo historia iliandikwa.
Meddie Kagere alitandaza mpira mwingi saaana akiwa Rayon Sports. Ikumbukwe kipindi hiki alikua bado hajaitwa timu ya Taifa ya Uganda. Kwa soka alilokua akilitandaza alisababisha maandamano makubwa sana nchini kwake, si toka kwa mashabiki wa Rayon Sports tu bali hata wapinzani wao wakubwa APR wote wakishinikiza apewe uraia fasta ili aweze kuitumikia timu ya Taifa ya Rwanda (ingekua Bongo mashabiki wa Simba SC na Ndala tushinikize Asante Kwasi apewe uraia wa Tanzania).
Nasikia Rais Paul Kagame asingekua makini, haya maandamano yalikua yanamuondoa madarakani. Hatimae mwaka 2014 Meddie Kagere alikabidhiwa uraia wa Rwanda, na katika mechi ya kwanza jamaa alicheka na nyavu. Kilichofuata baada ya hapo ni historia.

Nikiripoti toka viyunga vya Kigali hapa Rwanda.. Ni Mimi sembo wa Simba TIIIIIIIIVIIIIIIIIIIIIIIIII (in George Malatu Voice)
 
sasa jamaa si ana miaka 37!!..hawatofaidi sana kipaji chake
Mkuu hao wenye miaka 20's wamefanya nini? Imagine kama sisi Simba SC tusharudisha hela yetu.. Vipi kuhusu Rwanda ambao wameanza kupata Huduma take tangu mwaka 2014?
 
mrudishe hela yenu ipi?..mmerudishaje?
Hela ya usajili Mkuu.. Kwa magoli anayofunga, tungekua na njaa kama mtaa wa 2, tungeenda kuchukua mkopo bank, na hayo magoli ikawa dhamana.. Au haya magoli yangekua ni guarantee tosha ya kupata wadhamini, kama tungetaka jezi zetu zingechafuka nembo mbali mbali.
 
Mkuu hao wenye miaka 20's wamefanya nini? Imagine kama sisi Simba SC tusharudisha hela yetu.. Vipi kuhusu Rwanda ambao wameanza kupata Huduma take tangu mwaka 2014?
Ndoto za mchana hizo
 
Hela ya usajili Mkuu.. Kwa magoli anayofunga, tungekua na njaa kama mtaa wa 2, tungeenda kuchukua mkopo bank, na hayo magoli ikawa dhamana.. Au haya magoli yangekua ni guarantee tosha ya kupata wadhamini, kama tungetaka jezi zetu zingechafuka nembo mbali mbali.
mtaa wa pili mtawakoma..mnawachukulia poa
 
Safi, watanzania tuige hii. sio wachezaji wazuri wanakuja tu kucheza ligi na huko kwao hawaitwi kwanini tusiwatumie? mbona nchi za weenzetu hat ulaya wanafanya hivyo?
 
hahahaahah maandamano ya soka yamuondoe Kagame mkuu hahahahaha alafu usiseme simba na ndala hapo sema mkia na ndala hamna timu hapo....kungekuwa na timu taifa stars ingekuwa mbali
 
hahahaahah maandamano ya soka yamuondoe Kagame mkuu hahahahaha alafu usiseme simba na ndala hapo sema mkia na ndala hamna timu hapo....kungekuwa na timu taifa stars ingekuwa mbali

Hahaha.. Huwezi amini Mkuu ilibakia kidogo jamaa ang'oke.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom