Maandamano ya Mnyika yakwama

Maandamano ya Mnyika yakwama

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MAANDAMANO yaliyoandaliwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), yamegonga mwamba kutokana na kuahirishwa, baada ya askari polisi waliokuwa na mabomu ya machozi kuyazuia. Licha ya askari hao kuzuia maandamano hayo waliruhusu mbunge huyo kuhutubia wananchi waliofika eneo la Manzese, Bakheresa. Tanzania Daima ilishuhudia wananchi wakirushiana maneno mara kwa mara na askari waliokuwepo katika eneo hilo.

Askari hao wa kutuliza ghasia walikuwa katika gari namba PT 1524, PT 0890, M 672 CAH na PT 1902. Katika hali isiyo ya kawaida askari mmoja alisikika akiwaambia wananchi waondoke katika eneo hilo, kwani mabomu yakianza kurushwa watawavunja miguu, wakati huo mbunge akiwa anaendelea kula kuku kwa kuwa atakuwa hajaumia.

"Kwanza tunawachelewesha nini hawa tuwavuruge tu," alisikika askari huyo akisema. Akihutubia mkutano huo, Mnyika alisema kuwa ni lazima hoja inayohusu masuala ya maji ipatiwe ufumbuzi. "Leo hatutaandamana, lakini maandamano yatakuwepo baada ya kuwasilisha barua ya kukata rufaa kwa Waziri Nchimbi na tutataka kauli zao," alisema.

Mnyika alisema kuwa Machi 18, mwaka huu atapeleka barua ya kukata rufaa ya kuzuia maandamano ambapo watahitaji kauli za mawaziri hao kutolewa hadi ifikapo Machi 22, kabla hawajaamua kuandamana tena. Mnyika pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanaomba kujiunga na mabaraza ya katiba ili kupata wawakilishi bora watakaoongoza ikiwamo kuhakikisha Katiba mpya na bora itakayotetea masilahi ya wananchi inapatikana.

"Tuombe kushiriki katika mabaraza ya katiba ili tupate katiba itakayohakikisha haki za msingi zinalindwa," alisema. Awali Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Charles Kenyela, alikataza maandamano na mkutano huo, ambapo alitoa sababu mbalimbali ikiwamo eneo hilo la Manzese Bakhresa kutumika kwa maegesho ya magari ya mizigo.
 
Nguvu ya Umma inaogopa bomu la machozi na maji ya kuwasha! mnashindwa hata na wafuasi wa Ponda walioandamana kiaina bila kuogopa!
 
Nguvu ya Umma inaogopa bomu la machozi na maji ya kuwasha! mnashindwa hata na wafuasi wa Ponda walioandamana kiaina bila kuogopa!

Kadogoo,

Nguvu ya umma ipo wapi? Nguvu ya umma wabunge 24.
 
Nguvu ya Umma inaogopa bomu la machozi na maji ya kuwasha! mnashindwa hata na wafuasi wa Ponda walioandamana kiaina bila kuogopa!
Wakitii sheria wameogopa, wakilazimisha hawatii sheria, lipi jema enyi magamba maccm
 
Kumbe muda mwingine hizi ID zina sadifu yaliyomo kichwani mwa mtu kumbe kweli we ni Kadogoo!
Nguvu ya Umma inaogopa bomu la machozi na maji ya kuwasha! mnashindwa hata na wafuasi wa Ponda walioandamana kiaina bila kuogopa!
 
Last edited by a moderator:
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"]

[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]

[TD="bgcolor: #ffffff"]
[/TD]
[TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
Awali Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Charles Kenyela, alikataza maandamano na mkutano huo, ambapo alitoa sababu mbalimbali ikiwamo eneo hilo la Manzese Bakhresa kutumika kwa maegesho ya magari ya mizigo.

[/TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kamanda wa Wilaya ya Kinondoni!
 
Nazipenda sana Siasa za Mbunge Mnyika. Anajenga nguvu ya hoja na kuisimamia katika sheria hizi hizi zinazobainishwa na baadhi ya watu kama kandamizi badala ya hoja za nguvu kama wanasiasa wengine.

Wanasiasa wengine wanatafuta umaarufu kwa kuvuja sheria wakati yeye anapata umaarufu kwa kujenga hoja inayosimamiwa na nguvu ya hoja. Siyo ajabu kama angekuwa mwanasiasa mwingine angehimiza maandamano yafanyike kwa nguvu bila kujari athari zake huku wakidai kuwa haki haipewi bali inadaiwa kwa nguvu.

I just wish, Tanzania ingekuwa na wanasiasa wengi kama Mh.Mnyika.
 
Ponda hana wafuasi, bali kuna waislam wanaotetea maslahi yao! hivyo nguvu ya wafuasi wa chadema huwezi kufananisha na ya waislam. acheni kujichanganya!
 
namsifu kwakuwa alisoma upepo na kusitisha maandamano. kilichopo sasa hivi kwa vijana wakova kama mkilazimisha maandamano bila kibali ni kuvunja miguu ili kesho mshindwe kuandamana. hiyo itakuwa nzuri.
 
Safi sana hii ndo inaitwa utii wa sheria bila shuruti
 
Wakitii sheria wameogopa, wakilazimisha hawatii sheria, lipi jema enyi magamba maccm
Tangu lini Nguvu ya Umma imetii sheria? kama ingekuwa hivyo Hosni Mubaraka na Kanal Gaddafi leo wangekuwa bado wako madarakani!
Kama hamna nguvu ya Umma mnapaswa kufunga midomo na kuendelea kutii sheria lakini msidanganye wananchi!
 
hahahaha....hao askari wa kutuliza ghasia ni kama mbwa wakali waliofungiwa kwa muda mrefu, huku wakiwa na hamu ya kung'ata nyama ya kiumbe kama mwanadamu. Acheni kabisa kujaribu mziki wa hao askari wa kutuliza ghasia kwa mgongo wa nguvu ya umma.
 
Nguvu ya Umma inaogopa bomu la machozi na maji ya kuwasha! mnashindwa hata na wafuasi wa Ponda walioandamana kiaina bila kuogopa!

we ---- ponda ameingiaje humu? kwa taarifa yako ponda hana wafuasi bali kuna waislamu.
 
Yote yana mwisho,kuna cku tu watakosa sababu za kuzuia na kukwamisha harakati za ukombozi.
 
cdm mna maeneo yenu ya kuandamana na c dar,kumbukeni hata ya yale ya kuwapokea wabunge wenu pale tzra kuelekea m/yanga nayo mlifeli au mmesahau
 
Back
Top Bottom