Maandamano ya madaktari yazuiwa

Maandamano ya madaktari yazuiwa

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
10,965
Reaction score
5,344
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limepiga marufuku maandamano ya madaktari yaliyopangwa kufanyika Jumatatu ijayo kushinikiza mambo kadhaa ikiwamo kuundwa tume huru ya kuchunguza kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa maandamano hayo hayatafanyika kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kiusalama.

Alisema wamesitisha maandamano hayo kwa sababu madai ya madaktari tayari yameshashughulikiwa na Serikali.

“Tumesitisha maandamano kwa sababu tunahofia kunaweza kutokea uvunjifu wa amani maana Waislamu nao walipanga kuandamana kesho (leo),” alisema Kova.

Msimamo wa madaktari

Kauli hiyo ya Kova ilitolewa saa chache baada ya kikao cha zaidi ya madaktari 400 waliokutana katika mkutano wa dharura ulioitishwa na Chama cha Madaktari (MAT), ambako waliridhia kufanyika kwa maandamano hayo.

Katibu wa (MAT) Dk Rodrick Kabangila alisema katika kikao hicho, madaktari hao walipokea taarifa ya MAT iliyoeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya wenzao waliofukuzwa.

“Madaktari wamepokea taarifa za wenzao kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji, ikiwamo kufukuzwa katika makazi yao kwa kutumia Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), kunyimwa chakula, posho na kuelezea kuwa vitendo hivyo ni vya unyanyasaji na uonevu dhidi ya taalamu na udaktari wenyewe,” alisema Dk Kabangila.

Dk Kabangila alisema kuwa, kufuatia hatua hiyo madaktari hao wamepitisha azimio la kufanya maandamano ya amani ambayo yanatarajia kushirikisha madaktari zaidi ya 800 hadi 1,000 na kutoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema na taaluma hiyo, kushiriki wakiwa na vitambaa vyeupe.

Akizungumzia msimamo wa polisi kuyazuia maandamano hayo, Dk Kabangila alisema uongozi wa madaktari utakutana kujadili tamko hilo la polisi.

“Tumepata barua inayozuia maandamano yetu. Barua hii imetoa sababu ambazo ni tofauti na sisi tulichoomba. Sisi (MAT) ndio tulioomba maandamano kwa ajili ya kuonyesha hisia zetu juu ya vitendo wanavyofanyiwa madaktari,” alisema Dk Kabangila.
 
Hao madaktari waliofukuzwa kwenye nyumba na FFU wamejitakia. Muajili wao alikwisha waambia waache kazi na waondoke kwenye nyumba za mwajili sasa wao wanasubiri nini?
 
Huo ni uonevu mkubwa,Nakwambia nchi hii inaendeshwa na mabavu sana akili ndogo tu inatumika!
 
Huo ni uonevu mkubwa,Nakwambia nchi hii inaendeshwa na mabavu sana akili ndogo tu inatumika!
Have always known Kova to have physical disabilities and never knew that he had also psychological disability. With his kind you can never expect intelligent actions. It is not that they have power it just that their time has not come. It is people who win wars not armies.
 
whoever you are tumia akili usiwe masikini wa fikra hata kama wewe ni jk au kova hayo ni madaraka tu umepewa, ipo siku utayaacha nafsi yako ndiyo itakuwa shahidi wa kwanza kukusuta
 
Back
Top Bottom