comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Kutokana umasiki kuzidi, kukosa vyakula, umeme, madawa hospitalini na unyanyasaji wanaofanyiwa na taasisi za kisheria kwa wananchi wake, wananchi nchini Venezuela wameendelea na maandamano makubwa katika mji kadhaa wakimtaka Rais wa nchi hiyo Nicola's Maduro aachie madaraka na aondoke Ikulu ya nch hiyo, tangu Maduro aingie madarakani nchini Venezuela amekua na sera mbovu za uchumi na sheria, maandamano hayo yamechochewa zaidi na kitendo cha Mahakama Kuu nchini Venezuela kutaka kupokonya nguvu ya kibunge katika Bunge la Venezuela licha ya jaribio la mahakama kuu kugonga mwamba lakini maandamanao ndio yamezidi kupamba moto, polisi nchini Venezuela wanapambana na nguvu kubwa ya waandamanaji, mmoja wa Kiongozi wa upinzani wa kisisasa nchini humo ndugu Freddy Guevara ameyaita maandamano hayo ni " mapambano ya kujihami" zaidi kisiasa, hali katika mji mkuu wa nchi hiyo Caracass sio shwari kwani vituo vya usafiri na mafuta vimefungwa kuhofia vurugu zaidi nchini humo
BBC
BBC