Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,889
Maandamano ya wapinzani miaka ya yuma yalisaidia sana katika kutafuta haki na usawa japo yaliambatana na madhara mbalimbali(kila mtu anayajua).
Leo hii mambo ni tofauti na hali pia ni tofauti kabisa.Kuna watu wame-take advantage ya hali hii na bahati mbaya sana wapinzani hawakuwahi hata siku moja kwenda Mahakamani kudai haki yao ya kikatiba ya kuandamana.
Kibaya zaidi,hivi sasa hata mikutano ya kisiasa nayo inaanza kudoda. Hakika hii ni hatari sana kwa ustawi wa upinzani nchini.
Athari inayoanza kujitojeza kwa sasa ni kuwa,nguvu ya upinzani nchini imebaki ndani ya Bunge tu na Bunge likiisha upinzani nao unakuwa kimya jumla!Hakika huku ni kujichimbia kaburi na ni faida kwa chama tawala.
Haki ya kuandamana na kufanya mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba na wapinzani ikibidi muitafute haki hiyo Mahakamani pale mnapozuiwa kama mlivyofanya katika kutafuta haki ya kumzika marehemu kamanda Mawazo.
Upinzani wa CHADEMA wa leo ni tofauti sana na ule upinzani wa miaka ya 2012 kurudi nyuma.Zi wapi operation Sangara leo hii?M4C leo hii iko wapi?Press conference za chama leo hii ziko wapi?Matamko ya chama leo yako wapi?
Vivyo hivyo,upinzani wa CUF wa leo ni tofauti sana na ule upinzani wa miaka ya 2000 kurudi nyuma.Serikali ya Umoja wa Kitaifa leo hii ndio imebadili kabisa siasa na harakati za CUF?

Last edited: