Ndio Polisi wetu walivyo. Sie mtaani kwetu kulikuwa na kibaka sugu mmoja na kundi lake walikuwa wanasumbua sana. Kila siku wakipelekwa Polisi wanatoka. Mpaka siku moja wakamvamia dada wa mkuu wa kituo kidogo cha polisi hapa mtaani. Hapo ndio walikamatwa wakafikishwa mahakamani na huyo afande Mkuu wa Kituo akaorganize mashahidi wa kutosha jamaa akahesabiwa mvua 125 kwa makosa mbali mbali ya mpaka miaka mitatu iliyopita. Sasa hivi anaozea Segerea, na chama lake lote wametawanyika mtaa uko salama.