Display Name
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 423
- 451
Uhuru ni hali ya mtu kuwa na nafasi kuongea, kufanya na kutafuta Amani bila kuingiliwa. Uhuru ni muhimu kwa kuwa una matokeo ya kuongeza ubunifu na mawazo ya mtu binafsi, kuongeza uzalishaji na kiboresha hali ya maisha kwa ujumla.
Ufafanuzi kuhusu neno Uhuru ni gumu kidogo na linahitaji kutafsiriwa na kutetewa kwa kizazi hata kizazi. Thamani ya Uhuru huthaminiwa na kueleweka zaidi na wale walioonja kutokuwepo kwa Uhuru.
Mara nyingi watu ambao wanaishi kipindi/muda ambao kuna Uhuru huchukulia mambo kirahisi, vivyohivyo wale ambao wamekuwepo/wameishi kipindi ambacho hakukuwa na Uhuru wamekuwa wakipata wakati mgumu kuelewa Uhuru kuuishi kwenye Jamii.
Hakuna aliye huru kabisa unapokuwa unaishi kwenye maeneo kama Miji au Nchi ambapo huwa kunakuwa na utawala wa Madaraka ya Kisiasa hivyo Uhuru hutegemeana na Haki ya Mtu na Wajibu na Malengo ya Eneo/Taifa husika. Kutokana na hilo, tunakuwa na Sheria, Kanuni na Matamko ya Kimahakama yanayotoa mwongozo kwenye namna Uhuru unatakiwa kuwepo.
Duniani, Nchi nyingi kwa umakini kabisa zimepokea/zimeasili nyaraka mbalimbali zinazofafanua tafsiri na kulinda Uhuru wao. Haki nyingi zinazotetewa zinaangukia kwenye Uhuru wa Kuabudu, Uhuru wa Kuongea, Uhuru wa Kukusanyika na Uhuru wa Kupinga/Kuikosoa Serikali