Pius J. Kiwarya Lema
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 1,097
- 567
Kwa miaka 41nimezaliwa wa nimeishi Tanzania Kilimanjaro Ninaijua historia :
Ukiona jambo linapotoshwa na watu wanaojitekenya wenyewe na kucheka wenyewe ni lazima usahihishe vinginevyo wanaweza kufuta maana njema ya jambo husika.
MTI wa ISALE au JANI lake lina maana moja tu ya ASILI nayo ni
"MPAKA' kati ya shamba lako eneo lako unakoishia .
Mmea huu unapandwa kwenye mpaka kuonyesha mwisho wa sehemu yako, ,kiwanja chako na si vinginevyo !
Kwa lugha ya Leo kwenye viwanja au shamba wanaweka jiwe .
Matumizi ya jani la Isale, yalishika kasi ya miaka 1800 kutokana na ujio wa wakoloni hasa wajerumani kwa nia ya kuwaonyesha himaya au tawala ya eneo fulani hivyo wakitaka kuingia ni lazima mazungumzo yawepo !
Kadri miaka ilivyosogea jani hili lilikuwa linatumika kuonyesha jambo alilonalo au ambavyo angependa lifanyike.
Mojawapo ya eneo ambalo Isale ilitumika hata (hata leo )kama Ishara ya kuonyesha jambo ni kupandwa mpakani mwa mashamba.hats kama hakuna ugomvi
Baadayev yakawa yanapamba gari Lililobeba Maiti kutoka Mochwari kuelezea au kuonyesha kwamba kuna jambo linaumiza limetokea ama linahitaji ufumbuzi !
Ushahidi mdogo wa Matumizi ya Jani Ia ISALE ni mwaka 1989 alipofariki Babu yangu Mzee Philemon(1900) Nlengu Muro MANAI Kiwarya Lema gari ilipambwa kwa masale pale mbele "!
Sasa niulize kwa hawa wapotoshaji wa sasa wanaodai lina Maana ya amani!
walikuwa wanataka amani nani ? Au walikuwa wamemkosea Nani?
Jani la Isale halibebwi tu kienyeji ,
Mtu makini akilibeba ataenda kuliweka mahali alikokusudia sio kuzunguka zunguka nalo barabarani !
Iwe kwenye shamba au kiwanja au nyumba au kupamba gari au ukumbi Wa shughuli husika lakini sio kama wafanyavyo wanasiasa wa siku hizi .
Napenda kuhitimisha Kuwa Jani hili linamaanisha kero aliyonayo mtu au uzuri alionao mtu au jambo alilonalo MTU Kwako lakini siyo kutaka amani au kuonyesha Furaha aliyonayo.
Amani ni matokeo ya kutatua hicho kilichomfanya aone mbele yako.
Furaha itakuwa ni matokeo kutatua kile kilichomfanya akuone kero .
Kwa hiyo siyo kila anayekuona kero na kubeba ISALE ana kero.
Siyo kila anayefurahia na kubeba ISALE ana furaha.
Cha kujifunza Isale ni Alama ya mpaka wa ardhi tu.Kama mpaka haupo Amani ya moyo haipo !
Mpaka wa shetani katika Ulimwengu Wa roho umeshaondolewa kwa Damu ya Yesu Kristo hivyo Isale linabaki kama kumbukumbu tu ya mmea wa Kihistoria uliotumika kulekeza ishara ya kutoingia kwenye himaya mtu mwingine
Kiwarya.JP.Lema