Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,177
- 7,301
Wengi wetu akili na mawazo ndio hutupa maana ya utu. Tukumbuke mawazo ni mkusanyiko wa kumbukumbu mbalimbali zilizohifadhiwa kwenye akili tulizozipata kwa kuona au kusikia.
Tukizingatia akili huhifadhi chochote kiwe kibaya kiwe kizuri. Na ndani ya akili ndimo hutoka baadhi ya mawazo yadanganyayo.
Ndani ya roho ya mtu mna ufahamu na huo ufahamu ndio utu. Ufahamu upo ngazi ya juu mno ukilinganisha na akili na kamwe akili haiwezi waza mambo ya ufahamu (Akili haina uwezo wa kujua maana ya utu) Ufahamu ndo ufanya moyo upige, macho yaone, usikie nk.
Ndani ya ufahamu hakuna chuki, wivu, majivuno, kusengenya na mambo yanayofanana na hayo MAANA HAYO NI MATENDO YA AKILI. Ndani ya ufahamu kuna SASA/LEO hakuna JANA wala KESHO.
Ukiamua kuishi LEO na kuachana na kutazama maana ya utu kwenye kioo cha JANA/WAKATI ULIOPITA INA maana uko huru 100% kuhusiana na vifungo na maumivu ya kihisia kama chuki maana chuki huambatana na mambo ambayo yalikwishapita. Ukiachana na kutazama maana ya utu kwa kitu utakachomiliki au nafasi utakayokuwa nayo WAKATI UJAO , utaachana na vifungo kama MSONGO WA MAWAZO ya mambo yajayo, kwasababu unayoyataka huna uhakika wala uwezo wa kuyafanya yawe kama utakavyo.
Je akili ina umuhimu gani?
Akili ni kifaa tu cha kumsaidia mtu kufanya baadhi ya mambo mfano kutusaidia kusoma, kuweka mipango ya kazi nk
Je tufanyeje ili kuishi katika ufahamu?
Ukiishi SASA/LEO unaishi kwa ufahamu maana hutatembea na vifungo kama chuki za jana/wakati uliopita wala msongo wa mawazo ya kesho.