Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Hello JF Fans.!
Leo ni siku ya Ibada hasa kwa Wakristo walio wengi, lakini bado kuna ambao hatuwezi kufika Kwenye sehemu za Kusanyiko kushiriki na wenzetu katika Ibada kutona na sababu kadha wa kadha.
Nami natumia fursa hii, kuwakumbusha hasa Wakristo wenzangu na kwa Neema za Mungu hata wasio Wakristo wanaweza kupata jambo muhimu la kujifunza siku ya leo.
Ujumbe wangu umejikita juu ya KIFO CHA MWANADAMU.
Tumezoea kusikia pale panapotokea mauti, watu walio wengi hata Wakristo wakisema, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Wengine wameenda mbali zaidi na kusema Yote ni Mapenzi ya Mungu. Hivyo, Vifo vyote vinavyotokea ni kwa sababu Mungu amependa.
Ni kwa muktadha huo, imepelekea kudadisi kwa kina jambo hili hasa kwa Misingi ya BIBLIA.
MAANA YA KIFO.
Mwanadamu ni Roho, Roho inayoishi katika Mwili. Roho ikiwa ndani ya Mwili, Mwanadamu huitwa Kiumbe hai. Roho ikiondoka, Mwanadamu huitwa Kiumbe Mfu. Sasa KIFO ni hali ya Roho kutengana na Mwili.
Hata hivyo, hii ni Tafsiri katika hali ya KIFO pale Roho inapotengana na Mwili.
Kiuhalisia, Mwanadamu ambaye ni Roho hafi, maana Roho haiwezi kufa, ila hujitenga tu na Mwili. Sisi Wanadamu ambao ni Roho, tutafufuliwa hapo baadae siku ya hukumu. Na watakaokuwa wamefanikiwa kuingia Mbinguni wataishi MBINGUNI Milele, watakaokuwa hawajafanikiwa, wao watatupwa kwenye Moto wa Milele.
Ifahamike kuwa, KIFO haikuwa sehemu ya maisha ya Mwanadamu. Mwanadamu alikusudiwa kuishi Milele. Kifo kilifuatia tu baada ya Mwanadamu kuwa muasi kwa Mungu.
Endapo Adam na Eva, wasingetenda makosa hapo awali, Kifo isingekuwa sehemu ya maisha ya Mwanadamu. Hebu tazama maandiko haya.
Mwanzo 3: 3 Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Mwanzo 3: 19, Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3:22 BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele.
Kwa ushahidi huo hapo juu, inaonesha wazi kuwa, KIFO ni kama sehemu ya adhabu kwa Mwanadamu. Imekuwa hivyo tangu awali na kuendelea hivyo mpaka YESU alipokuja Duniani, wakati wa Mitume na baada ya Mitume wale wa mwanzo.
Pamoja na kuwa kifo kipo, lakini Mwanadamu aliye mcha Mungu ameahidiwa kuishi miaka mingi zaidi. Tangu enzi za Awali, Wanadamu walio wema waliishi maisha marefu na kufikia Uzee wao.
Hebu tazama baadhi ya umri wa Wanadamu wa Kale katika BIBLIA.
Adam aliishi miaka 930 (Mwanzo 5:5)
Seth mwana wa Adam aliishi miaka 912 (Mwanzo 5:8)
Enosh aliishi miaka 905 (Mwanzo 5:11)
Ibrahimu aliishi miaka 175 (Mwa 27: 7).
Ishmael aliishi miaka 137 ( Mwa 27 : 17)
Isaka aliishi miaka 180 (Mwanzo 35: 28 ).
Siku za kuishi Yakobo zilikuwa 147 (Mwanzo 46 ).
Yusufu alikufa akiwa na umri wa miaka 110 (Mwa 50)
Lakini, inaonesha kuwa, kutokana na maasi aliyokuwa akiyatenda Mwanadamu, ndivyo siku zake zilivyokuwa zikipungua zaidi.
Mwanzo 6:3 "Basi, Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa yeye naye ni nyama; siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Baadae tunaona miaka ikipunguwa na kufikia themanini.
Zab 90: 10 Inasema " Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini.
Lakini, kwamapenzi ya Mungu, bado Mungu anaweza kukuongezea miaka mingi zaidi. Imeandikwa...
"Maana kwa msaada wangu,siku zako zitazidishwa,na miaka ya maisha yako itaongezwa" (Mithali 9: 11).
Imeandikwa pia katika ( Mithali 10: 27 ).
"Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu,Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa"
Swali la Msingi, Je Binadamu kufariki angali akiwa kijana mwenye nguvu ni Mapenzi ya Mungu kweli.? Katika kusoma kwangu BIBLIA, hakuna nilipoona Mungu akiahidi mwanadamu afariki akiwa kijana mwenye nguvu. Kila nilipokuwa nikisoma, nimeona Kifo cha ghafla kikitokea kwa Wanadamu kama tu sehemu ya adhabu kutokana na kukosea kwao. Hivyo hii ni changamoto kwetu kuwa, ukiishi kwa kufuata taratibu za Mungu, Mapenzi ya Mungu ni Mwanadamu kuishi miaka mingi, na iwapo Mwanadamu hatafuata mapenzi ya Mungu atafariki mapema zaidi.
Hebu tuangalie ushahidi hapa chini.
Kwa kuwa,kila andiko lafaa kwa mafundisho na lina pumzi ya BWANA kama ilivyoandikwa katika 2 timotheo 3:16, “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.
Hivyo basi, siku ya leo ili kufupisha andiko hili, naomba kujikita zaidi katika kitabu cha Mithali.
Kwanza kabisa, mtu mwema hawezi kuwa sawa na mtu asiye mwema. Mtu mwema ana upendeleo zaidi kwa Mungu kuliko asiye mwema. Hebu tazama ushahidi wa maandiko....
"Mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA" ( Mithali 12 :2)
Hivyo, hapa chini nimejaribu kubainisha sababu sita(6) za Mwanadamu mwenye haki kuwa na haki ya kuishi siku nyingi na siku chache zaidi kwa Mwanadamu asiye na haki mbele za Mungu.
1. Wasiosikiliza kauli za Mungu.
"Mwanangu,sikiliza na kupokea kauli zangu, na miaka ya maisha yako itakuwa mingi" (Mithali 4: 10 ).
2. Wasio Haki mbele za Mungu.
"Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote , Bali wasio haki watajazwa mabaya" Mithali 12 : 21 ).
3. Wasiosikia Maonyo ya Mungu.
"Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.
Atakufa huyo kwa kukosa maonyo.Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake" ( Mithali 5 : 22 - 23).
4. Msiba wa Ghafla ni kwa Waovu tu.
"Mtu muovu,msiba wa ghafula utampata.Ghafula atavunjika,bila njia ya kupona" (Mithali 6 : 12 - 16 ).
5. Wanaomchukia Mungu.
Bali anikosaye hujidharau nafsi yake mwenyewe,na wao wanichukiao hupenda mauti ( Mithali 8: 36).
6. Wasiokuwa na Ufahamu wa Neno la Mungu.
Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu ( Mithali 10: 21).
Lakini, ifahamike kuwa, hapo awali vilitokea Vifo vya Watu wenye haki, bila shaka Mungu alikuwa na kusudi lake. Hata hivyo, kwa maoni yangu, nadhani na wao pia hawakufa wakiwa vijana, bali watu wazima.
Rejea Kifo cha Yohana Mbatizaji, aliyeuwawa kwa kukatwa kichwa. Rejea pia Kifo cha Mtume Stefano aliyeuwawa kwa kupigwa mawe. Ni maoni yangu kuwa, Vifo hivi vya wenye haki vilitokea ili kutimiza maneno ya YESU mwenyewe aliposema "Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehenum'' Mathayo 10: 28). Ni maoni yangu pia kuwa, Vifo hivi viliruhusiwa na Mungu kwa Wanadamu waliokuwa katika hali ya kupigania ukweli wa Mungu. Na kwamba, Mungu aliruhusu ili kuonesha kuwa, katika hali ya kulitetea NENO la Mungu, Mwanadamu awe tayari ikibidi hata kwa KIFO. Rejea pia baadhi ya msimamo wa Mtume Paul kuwa alikuwa tayari kufa kwa ajili ya YESU, na rejea pia msimamo wa akina Shadrack, Meshach na Abednego.
HITIMISHO.!
Mimi nami ni nani nipingane na maneno ya Mungu.? anayejiita Mkristo na anapingana na hoja hapo juu, atupe pia Ushahidi wa Kibiblia juu ya hoja zake.
Unaweza kujiuliza, kama Kifo katika hali ya kutokushiba umri hapa Duniani ni kwa ajili ya wasiotii maneno ya Mungu, iweje watoto wadogo wasiojua mema na mabaya wafe.? Hii ni hoja nyingine na inahitaji muda wake mwingine. Leo tuzungumzie Kifo katika muktadha wa wenye kumtii Mungu na Wasiomtii Mungu.
Unaweza pia kujiuliza, mbona flani amefariki akiwa kijana tu na alikuwa na bidii katika Mungu na Mcha Mungu. Jibu lake ni kuwa, ajuaye huyu ni Mcha Mungu ni Mungu mwenyewe, peke yake. Sisi Wanadamu hatuwezi kumjua Mcha Mungu wakweli. Hata mimi nayeandika hapa, ni Mungu pekee ajuaye kama ni Mcha Mungu au la.
Kwa ushahidi huo, huwa siafiki Watu wanaosema kuwa Vifo vya ajali, magonjwa ya kila namna hasa kwa vijana wenye nguvu ni Mapenzi ya Mungu. Hakuna ushahidi popote panapoonesha kuwa Mungu ameahidi kifo kwa kijana Mcha Mungu wa kweli. Bali KIFO haswa kile cha ghafla ni kwa ajili ya wasio mcha Mungu, kutokana na ushahidi wa maandiko hapo juu.
Baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha na karibuni kwa michango zaidi.