Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,231
Ni msamaha huo. Ila anaepusha shari za mbeleni.Je nikisamehe afu nisigeuke tena nlipokua? Mfano mi nawe marafiki umenikosea nimekusamehe tena kwa moyo mweupe ila sipo tayari tuwe marafiki tena kama zamani, huo ni msamaha? Au sijakidhi vigezo vya msamaha?
Ndio nduguuu.Mm nikushasamehe na namba nafuta kila kitu na kama upo mbal ndo nakusahau kabisaaa.. Nikikuona ni hello tuu ... Hapo nimesaheme in which perspective.... Lengo ni kuepuka possibility ya kurepeat the same mistake..
Hujasamehe. Sahau aliokufanyia utatua mzigo mzito sana. Mpe salamu yake kwakua anaitikia. Huwezi jua atakusaidia nini.Jamani Galacha mimi kunamtu alinikosea na nikamsamehe ila nikikutana naye salam tu bac ila nahic hata salam nisipe tena yaani kwa wastani bado moyo wangu unasumbuka na ule msamaha. Je nifanyaje.
Itabidi nijifunze tuuHujasamehe. Sahau aliokufanyia utatua mzigo mzito sana. Mpe salamu yake kwakua anaitikia. Huwezi jua atakusaidia nini.
Ndio ukiona hivo mpotezee.Ukimsamehe mtu ni bora ukae nae mbali sana ili kuepusha Shari lingine, pia wengine huwaga wanaombaga msamaha ili wapate chance yakukukomesha zaidi ya mwanzo.
Huo unaitwa ni msamaha wa masharti.Je nikisamehe afu nisigeuke tena nlipokua? Mfano mi nawe marafiki umenikosea nimekusamehe tena kwa moyo mweupe ila sipo tayari tuwe marafiki tena kama zamani, huo ni msamaha? Au sijakidhi vigezo vya msamaha?
Ni msamaha pia so long as huna kinyongo naye, coz hata kwenye bible daudi alikosea mungu alimsamehe lakini adhabu ilikuwa palepale ila baada ya adhabu mambo yakawa fresh huo ndio msamahaJe nikisamehe afu nisigeuke tena nlipokua? Mfano mi nawe marafiki umenikosea nimekusamehe tena kwa moyo mweupe ila sipo tayari tuwe marafiki tena kama zamani, huo ni msamaha? Au sijakidhi vigezo vya msamaha?
Samehe usamehewe.Inategemea na kosa lenyewe, makosa mengine hayanaga msamaha daima dumu
Mengine magumu kiongozi, we wacha tu. Na wakati mwingine kusamehe ni unafiki tu maana ukimuona aliyekukosea lazima lile jambo utalikumbuka. Mathalani binti yako kabakwa au mtoto wako kaliwa tigo halafu aliyemtenda mpo mtaa mmoja. Halafu kesi ilipopelekwa mahakamani akashinda kesi karudi mtaani, hivi mtu huyo utamsamehe na kuanza kuchat na kufurahi pamoja as if hakuna kilichojitokeza? Mimi nasema inategemeana na kosa lenyeweSamehe usamehewe.
Ntasamehe na kupita. Yanini kujiumiza. Hata nisiposamehe atapungukiwa na nini. Yanini nijiwekee mizigo mizito moyoni. Ishatokea.Mengine magumu kiongozi, we wacha tu. Na wakati mwingine kusamehe ni unafiki tu maana ukimuona aliyekukosea lazima lile jambo utalikumbuka. Mathalani binti yako kabakwa au mtoto wako kaliwa tigo halafu aliyemtenda mpo mtaa mmoja. Halafu kesi ilipopelekwa mahakamani akashinda kesi karudi mtaani, hivi mtu huyo utamsamehe na kuanza kuchat na kufurahi pamoja as if hakuna kilichojitokeza? Mimi nasema inategemeana na kosa lenyewe
Hayajakukuta mkuu, ila subiri ipo siku utajakumbuka haya maneno hapaNtasamehe na kupita. Yanini kujiumiza. Hata nisiposamehe atapungukiwa na nini. Yanini nijiwekee mizigo mizito moyoni. Ishatokea.
MAANA HALISI YA MSAMAHA
Msamaha ni pale ambapo mimi naamua kupoteza haki yangu ya kukuumiza wewe kwa kuniumiza mimi.
Unaposamehe unaepuka kutengeneza maumivu zaidi.
Amua leo kuwasamehe wote waliokuumiza, maana kuendelea kukaa na kinyongo unazidi kuumia wewe.
Mimi natangaza kusameheana na wote walionikosea na sintoweka kinyongo tena, wewe je?
Bonyeza Like kama wewe ni mtoa msamaha twende pamoja