Habari wana JF
Baada ya harusi niligundua Mke wangu anadate na cameraman wa harusi yetu, hii ilikuwa ni baada kufuma messages (conservation) wakati tupo honeymoon alipokwenda kuoga, inaonekana walikuwa wananichora tukiwa high table.
Sikumwambia chochote japo iliniuma nikapotezea kwa kuwa maji nilishayavulia nguo nikajua maybe baada ya pale wataachana maana mwamba atakuwa kashaamini kuwa tupo serious ndio maana tumeoana. Baada ya mwezi mmoja nikagundua kuwa mke wangu ana mimba ya miezi 3 na sikuwahi kulala nae kabla ya honeymoon Ila kabla ya kugundua kuwa ana mimba ya miezi mitatu nilikuwa nikihisi tu kuwa mke wangu ana mimba kwa kuwa niliziona dalili mbalimbali sikutaka kumuuliza ila kwanini kwa haraka vile yaani mwezi tu mtu ana dalili konk vile ila nilipotezea kwa kuwa nilijua kila mimba ina stail yake ngoja nisubir akifikia kuniambia ataniambia.
Ndipo siku moja nikagundua kuwa kweli ana mimba na tena ni ya miezi mitatu najua mnajiuliza nilijuaje kuwa ana mimba ya miezi 3.
Niligundua hilo baada ya kufuma tena messages(conservatins) nyingine aliposahau cm yake mezani baada ya kwenda sokoni. Alikuwa akichat na yuleyule cameraman. Inaonekana mwanaume alikuwa akiulizia kuhusu mimba ile inaendeleaje na mbinu zao jinsi watakavyoniuzia mbuzi kwenye gunia.
Mwanamke aliporudi nilijikausha japo nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba usiku wa siku ile baada ya mwanamke kulala nilikuwa mwenye mawazo sana na nakumbuka niliinua mkono juu nilitaka kumchoma kisu afie usingizini kwa kuwa nilikuwa na hasira mno ila niliweza kujizuia ndipo nikaamua kujitengenezea kitanzi nijinyongee sebleni usiku ule (ndio nilijiona mjinga kwa kuwa nilifikiri mke wangu ni muaminifu kwangu kabla ya ndoa kumbe alinizunguka na vipi kuhusu muda na gharama nilizozitumia kufanya harusi na kwanini hakutaka kuniambia ukweli na bado walipanga kunizunguka na cameraman)
Nilijiona sina hatia nikajionea huruma ikabidi nifanye maamuzi magumu ya haraka usiku ule niliandika talaka tatu zilizokuwa na maelezo yote na kuzituma kwa njia ya cm kwenda kwa wazazi wake nikavunja line kisha niliamua kumtoroka kiukweli nilimuachia kila kitu cha ndani nashukuru MUNGU kwa kuwa nyumba tuliyoishi ilikuwa sio ya gharama sana ni kama million 15 tu Vyumba viwili na Sebule ilikuwa jijini Arusha ila hati ninayo hadi sasa nakumbuka niliondoka na hati ya nyumba na nguo nilizozivaa pekee ilikuwa mwaka juzi 2018 mwezi wa 7 ndipo nikahamia Dar es Salaam ndipo mwaka 2019 nikabahatika kupata mke mwingine kipenzi changu mahabuba ambae baada ya kunizalia mtoto huyu nilie nae nilienda kuthibitisha kwa kumpima DNA nikagundua sijaibiwa na mimi na mke wangu mpya tunapendana sana na sasa tunatimiza miaka miwili ya ndoa yetu. Yule malaya hadi leo cjui anaendeleaje na cameraman wake.
Najua wengi mnajiuliza kwanini niliondoka na hati ya nyumba ila kwa leo sitowapa majibu ila niambieni je, nilifanya makosa kufanya maamuzi yale?