Baada ya serikali ya awamu ya tanokuja na kauli mbiu ya kutumbua majipu ni dhana nzuri hasa katika kuleta uwajibikaji katika utumishi wa umma lakini staili inayotumika itatutia hasara hasa za kuwafidia waathirika, mathalani nimeshuhudia kule Kusini waziri mkuu amemsimamisha daktari kazi baada ya kupewa tuhuma na ndugu wa mgonjwa kuwa ameombwa Tsh laki moja je, tuhuma kama hizo zinaweza vipi kuthibitishwa maana yule mama hakutoa taarifa sehemu yoyote ile mpaka alipoenda waziri mkuu hizo tuhuma zinathibitishwaje?
Kule Mwanza mkuu wa mkoa amewasimamisha na kuamuru kukamatwa kwa walimu nane (8)wa shule ya sekondari kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi na wanafunzi wao tuhuma hizo zinathibitishwaje maana sidhani kama ni wahanga wametoa malalamiko hayo isipokuwa huenda ni wanafunzi wengine au wazazi wanafunzi waliofanyiwa kitendo hicho wanapatikanaje, watakubali kwenda kuthibitisha mahakamani kuwa walikuwa wanafanyiwa hivyo na walimu wao na utapatikana ushahidi wa kimazingira na kidaktari kuthibitisha tuhuma hizo.
Ukweli ni kwamba Serikali itashindwa vibaya mno kwenye kesi hizo na hapo ndipo waathirika watafungua za kesi madai na serikali kuwalipa mamilioni ya pesa.
Tunaomba uweledi utumike katika kutumbua hayo majipu ili mwisho wa siku serikali isiingie hasara za kuwalipa fidia hao waathirika vile vile mamlaka za uajiri zipewe nafasi katika kushughulikia kesi kuliko hivi sasa ambapo wanasiasa wanajichukulia hatua bila kufuata taratibu za utumishi.