Maamuzi ya mtu kuua na kisha kujiua huku ukijua watoto watabaki duniani wakiteseka

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Wakuu, kumekuwa na matukio wakadha wa mtu kujiua, mtu kuua na kujiua aidha mchumba/mke wake, rafiki yake,wazazi wake kwa kutumia pastola au bunduki. Lakini hili la kuua na kujiua papo hapo limekuwa likishamili sana hapa kwetu Tanzania. Matukio yamekuwa mengi sana

Hasa wafanyabiashara, wanandoa, marafiki nk huku sababu kubwa zikiwa kama hazijulikani kiundani sana.

Take a look at this: Jinsi mume alivyomuua mke kwa risasi na yeye kujiua - Jinsi mume alivyomuua mke kwa risasi na yeye kujiua

Aua wanafamilia, ajiua kwa risasi Dar

http://www.habarileo.co.tz/index.ph...905-polisi-aua-mwenzake-ajiua-baada-ya-mechi#

POLISI AUA MWENZAKE KWA RISASI KISHA KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI KICHWANI | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Polisi aua kwa risasi akijiami | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Hizi ni baadhi tu ya habari zinazoonesha matukio mbalimbali ya mtu kuua na kisha kujiua.

Kwann baada ya kujiua,usimuache mwenzako Au kwann ukishaua wewe ubaki duniani kulea watoto na familia?

Ni sababu gani zinasababisha mtu kuua na kisha kujiua?Ni mambo ya kiimani au kisaikolojia?

Karibuni wakuu.
 
ni mengi tu yanachangia.wivu,ugomvi,kinyongo,na matatizo ya kisaikolojia.
na pia mengine ni spiritual problems.yani kama we aio mtu wa maombi na kujiweka karibu na mungu husali ukilala wala ukiamka wala kabla ya kula..ni rahisi kuingiwa na evil spirit..tena pepo la mauaji.
sasa likimvaa mtu utashangaa ghafla magomvi then anakimbilia bastola anakufumua bila kupoteza mda.lakini kuna hawa mapepo yanakutoka yakishafanikiwa kufanya wanalotaka.yani yule mtu akiahaua pepo nalo vuup!!linatoka na huyo mtu anarudiwa na sense zake,hapo ndo anaanza kujuta na akidikiria hakuna uwezekano wa yy kubaki huru..atasumbuliwa na mzimu wa aliyemuua bila hatia na hatokua na amani pia jela kifungo cha maisha kinamuhusu..sasa akifikiria hayo yote na ile hatia ya kuua inavomzonga roho yake lazima aone nae kufa ndo best option..
haiwezekani kubaki huru mtaani sababu ya watoto kwa mtu aliyeua.waachie ndugu wawalee.
 
Ndiyo hivyo ilivyopangwa toka kuzaliwa atakufa kwa kujiua ama kuuliwa. Kama haijapangwa hivyo piga ua hufi hivyo utakufa kifo kingine jinsi ulivyopangiwa
 
Kitendo cha mwanamke kurudi nyumbani usiku amelewa na mumewe kumfungulia mlango kinakera kweli, jamaa hakutaka ujinga.
 
Hivi kujiua ni uamzi wa kukaa na kujipanga? Mtua akae ikijipanga kama dili la namna ya kutoka kimaisha?
Shetani akikakaba, huwa hainaga ujanja, unapata hamu (lust to kill) kama upatavyo hamu ya kupiga mtu.
Sasa baada ya kutenda tukio, ndiyo shetani anakurejeshea akili zako. Hapo sasa ndiyo maamuzi magumu ya kudhuru nafsi yanapotokea, hasa mtu anapowaza mustakabali wake kuanzia kuswendemwa na wagambo kisha kufia jela kifo cha aibu.
 
Back
Top Bottom