Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,902
Kumekua na malalamiko ya chini chini na mengine ya wazi kabisa pale hatua zinapochukuliwa na mh. Rais au wateule wake kwa watendaji walioonesha kukengeuka miiko ya utumishi wa uma.
Mara zote hatu zimekua zikichukuliwa kwa makosa ambayo huainishwa na kwa kuyaangalia utaona kwamba maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya wahusika yalikua ni sahihi.
Sheria za ajira zinatuelekeza kwamba ili mwajiri aweze kufanya uchunguzi wake dhidi ya mwajiriwa ambaye ni mtuhumiwa anaweza kumsimamisha ajira yake ili kuweza kupata nafasi ya kufanya uchunguzi wake kwani mhusika akiwa ofisini anaweza kuvuruga uchunguzi dhidi yake kwa kuondoa ushahidi muhimu, hii ni hatua ya kwanza na muhimu.
Baada ya hapo, uchunguzi ukikamilika anaweza kuitwa ndani ya kikao cha maadili na kupewa muda wa kuzijibu tuhuma zake, kikao cha maadili kitaamua kusitisha ajira ya mhusika pale ambapo itabainika kua utetezi wake haukukidhi matakwa ya kikao.
Kama mtuhumiwa hakuridhika na maamuzi ya kikao anaweza kukata rufaa kwa ngazi ya juu ya utumishi kulingana na muongozo wa ajira unavyoeleza.
Ngazi ya juu ya maamuzi ikiamua kushikilia msimamo wa kikao cha kwanza basi ajira ya mhusika inakua imesitishwa rasmi ambapo sasa mwajiriwa anayohaki ya kupeleka shauri lake kwenye tume ya usuluhishi wa migogoro ya ajira.
Sasa, sina uhakika hao wote waliosimamishwa kama hatua nyingine nilizotaja zimeshachukuliwa, ila kwa kusikia wote tumeona kua kilichofanyika ni hatua ya mwanzo ni kusimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma.
Kama tuhuma ni ufisadi unaopelekea nchi kupoteza mapato yake hilo ni jambo jema na sahihi kufanyika.
Ni sahihi kabisa kumsimamisha mfanyakazi yoyote kama kuna tuhuma zinazoelekezwa juu yake, hii ni faida kwa mwajiri na kwake pia , kwani baada ya uchunguzi kukamilika matokeo yake yanaweza kumwondoa na hatia ambayo pia ingeweza kumchafua kwa jamii inayomzunguka.
Ni jambo sahihi kabisa kuhakikisha kua watendaji wa serikali wanapeleka fedha kwa kiwango na muda unaotakiwa katika miradi ineyolengwa.
Kumekua na ucheleweshwaji mkubwa wa kukamilika kwa miradi mingi ya serikali kutokana na sababu za ukosefu wa fedha au miradi kufanyika chini ya kiwango.
Kumekua na tabia ya muda mrefu kwa watumishi wa uma kuzidisha gharama za miradi mbali mbali ili kujipatia fedha.
Kuingia mikataba mibovu na tata. Yote hayo yamekua yakifanyika kwa miaka mingi. Sidhani kama ni sahihi tukiendelea na utaratibu huu.
Hatua zinazochukuliwa na nyingine zinazoendelea kuchukuliwa zinaweza zisiwafurahishe wahusika na wale waliokua wakifaidi kwa namna moja ama nyingine na utendaji mbovu wa watumishi wa uma, lakini wengi wetu tunaona ni sahihi kabisa.
Ni sahihi kabisa kama makusanyo na matumizi ya fedha za uma yakifanyika kwa usahihi.
Sijaona nchi yoyote duniani ikiendelea kwa kufanya maamuzi ya kufurahishana, mara zote maamuzi sahihi huipeleka taasisi au taifa mbele kimaendeleo.
Hivyo ni rai yangu kuona tukitoa support kwa maamuzi sahihi yanayofanyika na yatakayofanyika badala ya kusubiri kufanya maamuzi ya kufurashishana hatutaenda kokote.