Maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu yaendelea kupungua

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Ummy Mwalimu.jpg



Maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini yameendelea kupungua ambapo takwimu za mwezi wa Aprili 2016 zinaonesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 1,037, sawa na punguzo la asilimia 65 kutoka wagonjwa 2,953 walioripotiwa mwezi Machi 2016.

Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Wazir wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, amesema kuwa katika mwezi huu wa Aprili 2016, idadi ya wagonjwa imekuwa ikipungua kila wiki kutoka 368 wiki ya kwanza, 212 wiki ya pili, 143 wiki ya tatu hadi 104 wiki ya nne.

Ameitaja mikoa iliyoongoza kuwa na wagonjwa wapya wengi zaidi mwezi Aprili ni Mara (270), Kilimanjaro (198), Morogoro (188) na Dar-es-Salaam (90).

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa mwezi Aprili ni 16, wakati vifo vilivyoripotiwa mwezi Machi vilikuwa 47 ikiwa ni idadi pungufu kutoka asilimia 1.6 ya waliougua mwezi Machi hadi asilimia 1.5 ya waliougua mwezi Aprili.

Amesema pia takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia tarehe 1 Mei 2016, jumla ya wagonjwa 21,124 wametolewa taarifa na kati ya hao 331 wamepoteza maisha tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka 2015.

Waziri Mwalimu amesema kuwa licha ya kuwa na mwenendo chanya katika kasi ya kupungua kwa ugonjwa huu, bado kuna mikoa inayohitaji kuongeza juhudi zaidi katika mapambano haya.

Mikoa hiyo ni Morogoro, Kilimanjaro, Mara, Pwani na Dar-es-Salaam, ambapo ugonjwa huu umedumu kwa muda mrefu zaidi.

Amesema katika mikoa hiyowizara inaendelea kupeleka timu kutoka ngazi ya taifa kwa ajili ya kushirikiana na timu zilizopo mkoani na wilayani ili kuongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na tatizo hili.

Ni mikoa ya Njombe na Ruvuma tu ambayo haijaripoti mgonjwa yeyote wa Kipindupindu tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom