Maalim ziarani Mkoani Kilwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim ziarani Mkoani Kilwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Dec 13, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180

  [​IMG]

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Hoteli Tatu wilayani Kilwa baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Ludovick Mwananzila na kulia ni mfuasi wa CUF na mfuasi wa CCM.

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya afya kutokana na umuhimu wake kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla. Kauli hiyo imetolwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akingumza na wananchi wa kijiji cha Hoteli tatu Wilaya ya Kilwa, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho.

  Amesema taifa lenye maendeleo linategemea sana afya ya watu wake ambao ndio nguvu kazi, na ndio maana serikali imeandaa mpango maalum wa kuisogeza huduma hiyo kwa jamii kwa kujenga vituo vya afya karibu na makazi ya wananchi ili kuwaondoshea usumbufu.Maalim Seif ameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupeleka madaktari na wa uguzi wenye sifa mara kituo hicho kitakapokamilika ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kutokana na kufuata huduma hiyo masafa marefu.

  Aidha amewaasa wananchi wa kijiji hicho kuvitumia vituo vya afya kwa kupata matibabu sahihi, badala ya kuendelea kuwatumia waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kujaribu kuwapatia matibabu bila ya kutumia vipimo vyovyote.

  "Wakati wa kwenda kwa mganga ukapiga bao (yaani ramli) umepita sasa, huu ni wakati wa sayansi na teknolojia, tafadhalini tumieni vituo vyenu vya afya kujitafutia matibabu", aliasa Maalim Seif ambaye aliahidi kuchangia shilingi milioni moja kusaidia zahanati hiyo iweze kukamilika kwa haraka na kutoa huduma kwa wananchi.

  Nae Mkuu wa Wilaya ya Kilwa bw. Noordin Hassan Babu amewapongeza wananchi wa kijiji cha Hoteli tatu kwa kubuni mradi wa kujenga zahati hiyo ambao ni muhimu kwa maendeleo yao.Amesema serikali inaunga mkono juhudi hizo zinazoanzishwa na wananchi ikiwa na lengo la kujenga zahanati katika kila kijiji, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wananchi.

  Wakati huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye yuko Wilayani Kilwa kwa ziara ya siku nne alitembelea shughuli za Chama hicho na kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CUF kata ya Kipatimu na kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Chumo.Akizungumza na wanachama na wananchi wa vijiji hivyo, Katibu huyo Mkuu wa Chama Cha CUF amesema Chama hicho bado ni chama cha upinzani bara na visiwani, tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya watu kuwa kimekuwa CCM ‘B'.

  Amesema kuingia katika serikali kwa chama hicho haina maana kuwa kimegeuka kuwa CCM na kufafanua kuwa kila chama kina sera zake."Hatujaunganisha vyama, kila chama kina sera zake, nataka mfahamu wananchi wa Chumo kuwa CUF imeamua kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwa lengo la kunusuru maisha ya wanachi, na huu ndio mfumo unaotumika katika nchi mbali mbali sasa kwa vya kushirikiana kuunda serikali. Sio jambo la ajabu kabisa.

  Hivi hawa jamaa zetu wakitaka sisi kule Zanzibar tuendelee kuuwana kila siku? Alihoji.Amewata wananchi wa vijiji hivyo kukiunga mkono Chama Cha CUF ili kiweze kuwaletea maendeleo ya haraka kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili ikiwa ni pamoja na kuangalia maslahi ya wakulima wa zao la korosho na ufuta kama ilivyofanywa kwa wakulima wa zao la Karafuu visiwani Zanzibar ambao wakipandishiwa bei kutoka shilingi 3000 hadi 15,000 kwa kilo.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hakuna mkoa unaoitwa kilwa
   
 3. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anamkimbia Hamad Rashid???
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Hivi kaenda huko kama Katibu wa CUF ama makamu rais wa znz? Makamu rais wa znz anatambulikaje na katiba ya Muungano?
   
 5. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kwa nini maalim Cuf yupo na viongozi wa CCM????
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hamad Rashid kamtoa usingizini Maalim kwani anahisi kuwa yaliyompata muanzilishi wa CUF [ MAPALALA] naye yanaweza kumfika!!
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ulale mahala pema unakositahili cuf
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hamad Rashid amesaidia kweli kukuamsha usingizini maalim..welcome again kwenye siasa
   
 9. e

  elly1978 Senior Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  CCM-B, mbona vitu vipo wazi kama nani hii ya mbuzi, mkia mfupi hautoshi kufunika,
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Unaona Matatizo ya CUF kutembelea Maeneo ya PWANI tu; kwanini asiende Bukoka, Magu, Maswa?
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  anasema serikali ya Mapinduzi itaimarisha afya kwani hiyo zahanati imejengwa na SMZ?
   
 12. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kichwa cha habari taaabu tupu, anachoongea maalimu akbraka braka tu. Shida tupu.
   
 13. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Udini utakumalizeni nyinyi
   
 14. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu yupo Tanzania.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Kweli ndoa inazidi kuimalika zamani walikuwa wanafanyia vichochoroni sasa ni kweupe pee.
   
 16. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sa ndo wanamtandikia vitenge kama kitchen party? afu kama mkutano wa balozi wa nyumba 10!
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Ebo... mkuu wewe vipi? Unamzuia mwanamke kutembea na mumewe?
   
 18. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamaa wa CCM anamcheki kwa dharau kinyama,halafu kibabu hicho cha kafu kama hakiaminiamini hivi,kwamba du sikuizi tunasiti tugeza kweli?
   
 19. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wasije sisi huku wanaume hatuvai magauni wala hatufugi ndevu na kuva visuruali viduchu
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwanaume asiye fuga ndevu ni sho.ga
   
Loading...