Maalim Seif: Siwezi kamwe kurudi CCM hii ya sasa

Maalim Seif: Siwezi kamwe kurudi CCM hii ya sasa

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,092
Reaction score
34,904
seif+px.jpg

Maalim: Sikuamua kuja upinzani, bali CCM walinisukuma kwenda upinzani. Kama wanavyofanya sasa kwa Mansour (Yussuf Himid), they do the same thing (wanafanya kitu kilekile) na Mansour anapitia process (njia) hizohizo. Mimi nimefukuzwa CCM na zikatafutwa sababu nikawekwa ndani bila kosa lolote.PICHA|MAKTABA



KWA UFUPI
Mfumo haukufafanuliwa vizuri katika Katiba. Katiba yetu imefafanua tu kwamba rais, makamu wake na mawaziri watapatikana vipi na kwa uwiano upi, lakini baada ya hapo kwenda chini Katiba haikueleza.

Ni mengi yamesemwa kuhusu mwanasiasa huyu, Maalim Seif Shariff Hamad ambaye kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Yeye, ameshikilia nyadhifa mbalimbali tangu akiwa chama tawala, CCM hadi sasa akiwa Chama cha Wananchi (CUF). Ni nini zaidi anacho Maalim Seif? Endelea…

Swali: Unapoelekea kumaliza kipindi chako cha uongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), ni changamoto gani umezipata?

Maalim: Tukumbuke kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ni mfumo mpya katika nchi yetu na hata katika kura za maoni kuwauliza Wazanzibari waukubali au waukatae, wapo walioukataa. Waliukataa kwa hofu tu maana mara nyingi ukianzisha jambo jipya watu wengi lazima wawe na hofu. Bahati nzuri, asilimia 66 wakakubali mfumo huu.

Tumeanza vizuri na tumepata mafanikio, lakini na changamoto zipo. Changamoto ya kwanza ni mfumo kuzoeleka kwa watu, watu kujua serikali hii itaendeshwa vipi. Walizoea chama kimoja kuongoza serikali, walihoji katika Baraza la Wawakilishi mambo yatakuwaje, na wapo waliodhani kuwa hatutafanikiwa.

Nashukuru chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na busara zake tumeweza kwa kiasi kikubwa kushinda changamoto nyingi.

Katika ngazi ya kitaifa, hasa katika uhusiano wa kikazi kati ya rais, makamu wake wawili na mawaziri uhusiano ni mazuri, tunapata tatizo tunapoanza kuteremka ngazi za chini.

Katika ngazi za chini watu wamezoea mfumo wa chama kimoja ambapo kila kitu ni CCM, kwa hiyo wengine wanaona shida kwamba tuna kiongozi kutoka CUF, lakini lazima ukubali hali halisi.

Mfumo haukufafanuliwa vizuri katika Katiba. Katiba yetu imefafanua tu kwamba rais, makamu wake na mawaziri watapatikana vipi na kwa uwiano upi, lakini baada ya hapo kwenda chini Katiba haikueleza.

Ukiangalia ngazi za chini wengi wanaoteuliwa, pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao wameteuliwa kwenye siasa, bado ni wanachama wa CCM na bado ni wajumbe wa kamati za siasa za CCM. Haya ni mambo ambayo tumeyaona na lazima tuyarekebishe.

Utakuta mkuu wa mkoa au wilaya anakwenda katika kikao cha CCM na anajisahau kabisa kuwa ni kiongozi wa serikali na hatakiwi kwenye siasa. Tumepata matatizo na masheha ambao ni kikwazo kikubwa kwa mafaniko ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na wanaona wao ni mawakala wa CCM na siyo watu wa Serikali.

Swali: Ulijisikiaje siku CCM wanakufukuza uanachama?

Maalim: Sikuamua kuja upinzani, bali CCM walinisukuma kwenda upinzani. Kama wanavyofanya sasa kwa Mansour (Yussuf Himid), they do the same thing (wanafanya kitu kilekile) na Mansour anapitia process (njia) hizohizo. Mimi nimefukuzwa CCM na zikatafutwa sababu nikawekwa ndani bila kosa lolote. Mansour hakutoka CCM, Mansour wamemfukuza CCM na kisa cha kumfukuza ni kitendo cha kuunga mkono mfumo wa serikali tatu na baada ya kufukuzwa akaona watu walio karibu na msimamo wake ni CUF, lakini hajajiunga na CUF. Lakini, kwenye mikutano ya CUF anakuja na kuhutubia, sasa wamemtia ndani, ila ipo siku watamtoa, lakini wamemfanya kuwa shujaa, they create heroes themselves (wao wanatengeneza mashujaa).
Nakumbua Mwalimu aliwahi kuulizwa na redio moja ya Ujerumani kwamba ana regret (anajutia) mambo gani mawili aliyoyafanya; akasema moja ni kuitambua Biafra na la pili ni kuwafukuza kina Seif, CCM. Usalama wa Taifa kutoka Bara ulimwambia Mwalimu usifanye makosa ya kuwafukuza hawa, usalama kutoka Zanzibar wakamwambia Mwalimu wafukuze na ndio utakuwa mwisho wao watapigwa mawe barabarani.

Kikao cha Dodoma kilichoitishwa kutuhukumu sisi kilikwenda mpaka saa 6.00 za usiku sababu siku ya pili Mwalimu Nyerere alikuwa anaondoka hivyo ilikuwa lazima tufukuzwe.

Mimi kufukuzwa hakuniuma na nikasema nitakuwa huru kwa sasa kuangalia mwelekeo wangu na hasa nilipoona nimepata support (siungwi mkono) ya Wazanzibar wengi. Never give up (kamwe usikate tamaa).

Swali: Kuna siku tutarajie unaweza kurudi CCM?

Maalim: CCM yenyewe hii! Hii siyo ile CCM yetu sisi ambayo Mwalimu alikuwa mwenyekiti, mzee Kawawa, katibu mkuu huku sekretarieti ikiwa na Kingunge Ngombale Mwiru, Salim Ahmed Salim, Mosses Nnauye na Alfred Tandau. Hiyo ndiyo ilikuwa CCM bwana. Siyo CCM hii ya sasa ya akina Nape.

Swali: Unafikiri mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa unaweza kufaa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano?

Maalim: Wala sina shaka yoyote na wala hakuna suluhisho. Kwa mivutano iliyopo Tanzania Bara sioni suluhisho jingine isipokuwa tukubali kwamba lazima tufike mahali tufanye kazi pamoja. Faida moja ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kuunganisha vipaji vya watu wengi.

Vipaji vipo katika nchi na ukiviunganisha kila mmoja anaona kuwa this is my government (hii ni serikali yangu). Watu wasiwe na wasiwasi kwamba Bunge litakuwa butu, si kweli sisi tuna uzoefu wa Baraza la Wawakilishi ambalo hivi sasa lina meno zaidi kuliko pale ambapo hatukuwa na upinzani.

Kwa sababu nini; mkiwa na vyama viwili, kinachoongoza serikali na cha upinzani, chama kinachoongoza serikali watakuja kutetea serikali yao hata kama watajua kama hii sera si sahihi.

Lakini, uzoefu tuliopata kwenye Baraza la Wawakilishi wao wanajua kuibomoa serikali tu na hawajui kama ni waziri kutoka chama changu. Wao wanachojua huyu ni waziri kafanya kosa na kuna upungufu wanasema wazi na wakati mwingine hupigwa kura na serikali huwa inakaribia kushindwa. Hata debate (mijadala) inakuwa mikali katika Baraza la Wawakilishi. Zanzibar hivi sasa kukiwa na Bunge na Baraza la Wawakilishi, majority people (watu wengi) wanasikiliza Baraza la Wawakilishi kutokana na kuwa na mijadala mizito.

Kwa hiyo nadhani hili ni suluhisho la matatizo na mivutano hasa kwa Tanzania Bara na tusisahau kwamba mambo yakifanikiwa Zanzibar na Bara yatafanikiwa pia. Swali: Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa unajumuisha vyama viwili vya siasa ndani ya serikali moja, kwa kuwa kila chama kina ilani yake ya uchaguzi, ni ilani ya chama kipi inayotumika?
Maalim: Hilo ni moja ya tatizo ambalo hatukulitazama vizuri wakati tunaandaa mawazo ya kufanya kazi pamoja na kwa sasa unatumika uzoefu tu kwamba rais ndiye mwenye mamlaka ya kutoa sera ya serikali, sasa rais anaongozwa na sera ya chama chake.

Niseme kwamba Rais (Dk Shein) alipochukua serikali alichokifanya wakati akilihutubia Baraza la Wawakilishi alieleza mwelekeo wa serikali yake kwa miaka mitano, yapo mambo alitoa katika ilani ya CUF.

Sasa tunapata matatizo katika utekelezaji kwa sababu CCM wanataka kila jambo la mafaniko lionekane limetokana na ilani yao, lakini jambo lililoshindwa hawasemi. Kuna mambo ambayo yalikuwa katika ilani ya CUF yametekelezwa vizuri.

Tunachoangalia mbele zaidi ni kuchukua mifano ya nchi nyingine ambazo ziliunda serikali na kuunda kamati ndogo ambayo inaangalia ilani zote mbili halafu wanachukua mazuri kutoka katika ilani zote mbili na kuyaunganisha katika kitu kinachoitwa minimum program. Serikali inasimamia minimum program (mipango michache) kwa hivyo tunadhani mbele ya safari tutaelekea huko.

Swali: Kuna madai kuwa ushirikiano wa CUF na CCM Zanzibar unadhoofisha upinzani, kuna ukweli wowote katika madai haya?

Maalim : Hata siku moja, kwanza watu wanaosaidia sana kujenga chama katika Baraza la Wawakilishi ni wawakilishi wenyewe. Wawakilishi wetu wa CUF wana sauti (they are very vocal) na wanazungumza kwa hoja na hata wananchi wengi wakiwa na matatizo yao wanawaendea wawakilishi wa CUF ili wawasemee katika Baraza la Wawakilishi.Pili, sisi siyo kwa sababu tupo katika serikali tutakaa tu, tunaendelea kufanya mikutano ya hadhara na kuendeleza sera zetu.

Swali: Kwa nafasi yako ya Makamu wa Kwanza wa Rais, unaweza kuichambua serikali kama ilivyokuwa awali?

Jibu: Unakuwa umefungwa kwa sababu upo ndani ya serikali kwa hiyo criticism zako zote unatakiwa uzitoe mnapokutana katika cabinet (baraza la mawaziri).

Sasa, kutokana na majukumu yangu inakuwa vigumu kutoka nje na kuanza kuipinga serikali.

Niliwahi kufanya mara moja tena kwa sababu maalumu. Baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu, mimi sikuwepo, ila niliporudi nikakuta hali mbaya na watu wanateswa na kupigwa, kwa kweli sikuvumilia nilisema hadharani na kukemea. Nina ruksa ya kuzungumza na Rais muda wowote na hata kuzungumza na Makamu wa Pili wa Rais kwa sababu yeye ndiye msimamizi wa shughuli za rais za kila siku na pale mambo hayatakwenda vizuri namwambia makamu hapa look at it (hebu liangalie hili).

Swali: Kwanini Chama cha CUF siku zote kipo chini ya CCM licha ya kuwepo kwa madai kuwa CUF huwa kinashinda katika Uchaguzi Mkuu? Maalim : Binafsi, maslahi ya wananchi yapo juu zaidi kuliko maslahi yangu binafsi, nikihisi naweza kuchukua uamuzi, lakini watu wengi wakapoteza maisha yao huwa nina sacrifice (najitoa) kuliko kuwaambia watu waingie barabarani. Najua wazi kuwa vikosi vimeshapewa amri ya piga ua, sasa kwa nini upoteze maisha ya watu 10 au 20 kwa kuingia madarakani tu?
Utafika wakati nitapata free and fair election (uchaguzi huru na wa haki) na uamuzi wa wananchi utaheshimiwa na tunaelekea huko sasa hivi.

Soma mahojiano zaidi Ndani ya habari katika toleo letu la kesho

Swali: Unaamini vipindi vyote ulivyogombea urais Zanzibar ulishinda?

Maalim: Hiyo haina mjadala na Wapemba wanasema hiyo haina ‘kitochi'.

Swali: Katika uchaguzi mara zote nne ulizoshiriki ni uchaguzi gani unaoamini kuwa ulishinda bila kitochi?

Maalim: Uchaguzi uliopita, yaani wa mwaka 2010 nilishinda. Hata matokeo yalivyotangazwa walisema Rais Shein kanipita kwa kura 3,000 lakini kuna watu zaidi ya 18,000 ambao wamenyimwa haki ya kupiga kura na more than 80 per cent of them (zaidi ya asilimia 80) ni supporters (mashabiki ) wa CUF.




Inaendelea ukitaka kusoma zaidi bonyeza hapa.Maalim Seif: Siwezi kamwe kurudi CCM hii ya sasa - Makala - mwananchi.co.tz
 
Back
Top Bottom