Siku zote Seif yupo kimaslahi zaidi, sijawahi muamini na siku zote msimamo wangu kuhusu yeye ni negative. Ishara za mwanzo ni pale alipokubaliwa kurudishiwa marupurupu yake kama Waziri Kiongozi Mstaafu, ni kuanzia pale msimamo wake ukawa wazi, hakuwa tena kelele.
Seif aliondoka CCM baada ya kukorofishana na magamba wenzake kwenye maslahi na sio kitu kingine, ndipo akakimbilia CUF alikokaribishwa vijana waanzilishi wakiwemo kina Msabaha. Amepata alichokuwa akikihangaikia miaka yote,a nacho ni maslahi yake, utukufu.
Kina Mangula waliuliza hivi serikali haiwezi mrudishia marupurupu yake, kwani walishabaini kuwa tatizo ni maslahi yake, wakakubaliana arudishiwe naye aliporudishiwa akalainika. Ikaja zamu ya JK, CCM wakathibitisha ulafi wa jamaa, wakamtengezea cheo, akakimbilia pasipo kuhoji, na kama ilivyoshuhudiwa baada ya kuapishwa tu akikimbilia DSM, kuwakoga kwamba sasa yeye ni Makamu wa Rais, ha ha ha!!!!
Huyo ndo Maalim Seif!