Maalim Seif ni tatizo CUF

ameshindwa kujenga chama bara ,analilia ruzuku ya zanzibar ,profesa gani huyu
 
Kwani yeye Seif amegombea mara ngapi anashindwa mnamuona Lipumba wote ni wa kupumzika
 

Sana kiongozi hilo umenena! Kamamtu kweli alitaka umoja huu uimalike, kwanini aondoke wkt huu? Ila ajuetu kwamba wa Tanzania waleo upeo wao uko juu. Wanajua ktk safari ya mamba kamahii kenge hawakoseni. Hiki ndokipindi chakujuana nani mamba mwenzetu na kenge wao niyupi. Hiyo michezo aliyocheza Lipumba niyakitoto sana tena niya kizamani mno eti. Nahodha kujitosa baharini haizuii chombo kuendelea na safari, viongozi wa Ukawa kazeni buti mtusongeshe mbele wananchi tukonyuma yenu.
 
Bora huyu lipumba alipo ondoka asitake tuharibia Ukawa ytu.
 

Daaah!! Magamba mnahaha sana aisee. Mtaongea kila aina ya utumbo ili eti msambaratishe UKAWA. Sasa kwataarifa yenu nihivi, ukawa inawatu makini, huyo msaliti mlompa hela mkidhani kuondoka kwake kutagawa watu kaondoka mwenyewe kama mlivomuona, hakufuatwa na hata mjusi wala hatakaa amege hata mtu mmoja kutoka Cuf wala ukawa. Ninachowaasa wana ukawa nikwamba kazeni buti, msiteteleke hata sekunde moja. Huo nimkakati wa ma Ccm wanaogopa huo moto wenu wakusimamisha mgombea mmoja ktk kilajimbo, wanajua hawatakaa watoke safari hii kwahiyo wanajaribu kununua watu wanadhani nimuhimu ndani ya Ukawa ili umoja huu udhoofike. Mnachopaswa kujua nikwamba bado wataendelea kurubuni wengi wenu humo, ila msikate tamaa. Wapo watu mtawapa majimbo kuwa wagombea, mwisho wasiku wataingia mitini kimizengwe ili wagombea wa Ccm wapite bila kupingwa. Ila sisi wananchi tunatambua kazi kubwa mnayofanya kwania yakujenga nchi, tunawasihi msikatishwe tamaa nahao wasaliti wachache. Kumbukeni msemo usemao {kwenye safari ya mamba kenge hawakosekani} Viva UKAWA.
 
 

Na ndio maana akaamua kukimbia aibu
 

Makele mbele;
Moto wa Makaidi unawachoma kweli kweli. Hawaka wala hawa simami. UKAWA unawatoa jasho kila usiku unapo ingia wanaomba jua lisitokee kwani mwisho wao unakuja fasta mno.
Tuliwaona uchaguzi uliopita jinsi walivyo furahia hata Lipumba kumpigia debe JK. Ati ni mwenzetu wa dini yetu. Tuliona jinsi ambavyo watu walinunuliwa wakajitoa sekunde ya mwisho ati mwingine kapita bila kupingwa. Tuliona jinsi ambavyo upinzani walinyang'anyana kura za wazi ambazo ndizo zingempeleka puta JK.
Leo, ccm hawakutegemea kuwa UKAWA ingelivuka vikwazo vya zile njuluku za BMK. Tumevuka na sasa tumevuka kikwazo cha mgombea mmoja kila jimbo ili kuwe na ushindani sawa.
Mbona tena matumbo moto?? Wamelishwa dawa ya kusafisha tumbo au ni nini?? UKAWA ni moto wa kuotea mbali. Viongozi mlo bakia; Chonde chonde ndugu zetu, waoneeni huruma Watanzania, mtufikishe kwenye ndoto yetu tarehe 25 Oktoba, 2015. Mkiisha tuvusha tarehe hiyo basi vunjaneni mataya kwa ngumi, ng'oaneni meno, lakini Mungu atawalipa mema. Mmepigania uhuru wa Mtanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…