Maalim Seif na wapambe wake kuhamia Chadema haitakuwa ajabu maana CUF Lipumba ndiyo inatambuliwa na Msajili na Tume, na kwa maana hiyo ndiyo wenye mamlaka ya kuamua mgombea gani asimame kwa tiketi ya CUF na kamwe (kwa kusudi maalumu), hawatathubutu kumpitisha Maalim na Wabunge wake kugombea Urais na Ubunge kwa tiketi ya CUF.
Kwa kuwa mgogoro wa CUF Lipumba na CUF Maalim uko mahakamani, ni wazi lazima upo upande utashinda kesi, iwapo CUF Lipumba watashinda, watawavua uanachama Seif na Wabunge wake uanachama na kwa siasa za Zanzibar, lazima Seif na wafuasi wake wagombee. Kwa hiyo hakuna namna. Lkn pia kwa mazingira ya sasa , bila wapinzani kuungana hawataweza ku-survive maana ni wazi kuna mkakati wa kuua upinzani, na ndani ya wapinzani kuna vibaraka wengi ambao sasa wanarudi CCM na kutoa fursa kwa wapinzani kubakiwa na wapinzani halisi ambao itawapasa kuunganisha nguvu ili waweze kupambana na dola na CCM.
Kwa maana hiyo, kuna uwezekano wa asilimia 75 kwa Maalim na wenzake kujiunga na Chadema ili waweze kusimama Zanzibar, ukizingatia kuwa Chadema haina msingi imara Zanzibar.
Kama upo mkakati wa makusudi kuisambaratisha CUF kutoka kwa dola na CCM, bila shaka watajuta sana iwapo Maalim na kundi lake wataenda Chadema. Ikumbukwe kuwa kwa siasa za Zanzibar, vyama vilivyopo ni kivuli cha vyama vikivyokuwepo kabla ya Mapinduzi ya 1964; ASP, ZPP, na ZNP, ni vyama vilevile vyenye majina mapya.
Vv