Maalim Seif: Muda ukifika nitazungumza

Maalim Seif: Muda ukifika nitazungumza

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,152
Reaction score
162,563
. Siku nne tangu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema, Hashim Juma kumkaribisha Maalim Seif kujiunga na chama hicho akimuahidi kupitishwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar, katibu mkuu huyo wa CUF amewajibu kwa maneno mafupi, “Muda ukifika nitazungumza.”
Baada ya kusema hayo alisema kwa sasa hayuko tayari kuzungumzia suala hilo.

“Siwezi kuzungumza na waandishi wa habari kwa sasa. Lakini muda ukifika nitawaita na kuzungumza,” alisema Maalim Seif kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar, Nassor Ahmad Mazrui.

Kauli hiyo ya Maalim Seif inashabihiana kidogo na iliyotolewa juzi na Mbunge wa Malindi kwa tiketi ya chama hicho, Ally Saleh ambaye alikaririwa na Mwananchi akisema wakati ukifika wataona cha kufanya alimradi wanabaki ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF yenyewe.

Saleh alisema hayo akijibu ombi la kiongozi huyo wa Chadema kwamba chama hicho kipo tayari pia kuwapa nafasi wabunge wote wa CUF endapo watajiunga nacho.

CUF ipo katika mgogoro ulioanza mwaka 2016, baada ya Profesa Lipumba kutangaza kurejea katika chama hicho, ikiwa ni mwaka mmoja alipojiondoa katika uenyekiti akisema anakuwa mwanachama wa kawaida kisha kutengeua uamuzi wake, licha ya mkutano mkuu kuikubali barua yake ya kujiuzulu.

Aidha, tamko hilo fupi la Maalim Seif linaonyesha dalili za kiongozi huyo kulegeza msimamo wake wa awali aliowahi kuutoa kwamba hawezi kuihama CUF.

Pia, hatua ya Maalim Seif kutakiwa Chadema imeonekana kumshtua Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Magdalena Sakaya ambaye yupo upande wa Profesa Lipumba na jana alimshauri aachane na mpango huo, badala yake atulie ili alinde heshima yake.

Sakaya alisema ingawa suala la kuhama ni hiari ya mtu, itakuwa jambo la ajabu kama Maalim ataamua kuhamia Chadema kisha kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kama alivyoombwa.

“Akienda Chadema hawezi kushinda nafasi hiyo... akigombea upande wa Chadema itakuwa ni miujiza yeye kuibuka kidedea kwa sababu chama hiki hakina nguvu Zanzibar,” alisema Sakaya.

“Mimi kama mwanaye na yeye ni baba, nina mshauri atulie tu ili ajenge heshima yake kwa sababu aliwashawahi kuwa kiongozi mkubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, (SMZ),” alisema.

Sakaya ambaye hivi sasa anakaimu ukatibu mkuu wa CUF baada ya Maalim kushindwa kuripoti makao makuu ya ofisi ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam kutokana na mgogoro uliopo, alisema endapo kiongozi huyo atakwenda Chadema atajiua kisiasa.

“Namuonea huruma ni bora atulie kuliko kumangamanga, lakini akienda kule (Chadema) ndipo kaburi lake la kisiasa lilipo. Itakuwa kichekesho cha mwaka, unaacha kuijenga nyumba yako unakwenda kuimarisha ya jirani,” alisema Sakaya.

Sakaya alidai kuwa wazee wa Chadema hawana nia ya dhati ya kumtaka Maalim, badala yake wanataka kujiimarisha wao na kwamba kiongozi huyo atakuwa kama ngazi ya wao kupandia ili mchakato huo ufanikiwa.

Chanzo:Mwananchi
 
Tunamkaribisha kama tulivyomkaribisha Edward Lowasaa. Namini hata Maalim naye ni jembe kama alivyo EDO. Sisi wote ni mashahidi tunaona jitihada na juhudi za Lowasa katika chama chetu. Anavyokipigania usiku na mchana. Karibu Maalimu
 
Anatangaza ushindi wake?? Maana nasikia ndo rais wa zenj,
 
Naunga mkono Maalim Seifu na Wana CUF Zanzibar, kutafuta Chama kipya cha kuungana nacho. CUF hivi sasa ni mateka wa CCM kwa usaliti wa Lipumba.

Jifunzeni Kenya, Chama hakijawahi kuwa kikwazo kwa ushindi wowote panapokuwa na political will.

Siasa ni agenda, sio chama. Waachieni CCM na Lipumba CUF yao, Songeni mbele, Hakuna mtakachopoteza zaidi ya huo umakamu wa kwanza na wizara mbili zisizo na tija kwenu.

CCM haiko tayari kwa vyovyote vile kuiona CUF Ikulu ya Zanzibar.
 
Nadhani endapo Maalim Seif atahamia CDM basi naamini mpasuko mkubwa sana utakuwa ndani ya CDM kwanin nasema hivi chadema haijawa well organized hasa visiwani sasa kumleta Seif nadhani haitokuwa na tija sana huku bara na hata visiwani. Maalim atulie siasa ya bongo haiwezi kubadilika kwa maana mwenye maamuzi anaamua bila kujali matokeo yakoje.
 
Maalim Seif na wapambe wake kuhamia Chadema haitakuwa ajabu maana CUF Lipumba ndiyo inatambuliwa na Msajili na Tume, na kwa maana hiyo ndiyo wenye mamlaka ya kuamua mgombea gani asimame kwa tiketi ya CUF na kamwe (kwa kusudi maalumu), hawatathubutu kumpitisha Maalim na Wabunge wake kugombea Urais na Ubunge kwa tiketi ya CUF.

Kwa kuwa mgogoro wa CUF Lipumba na CUF Maalim uko mahakamani, ni wazi lazima upo upande utashinda kesi, iwapo CUF Lipumba watashinda, watawavua uanachama Seif na Wabunge wake uanachama na kwa siasa za Zanzibar, lazima Seif na wafuasi wake wagombee. Kwa hiyo hakuna namna. Lkn pia kwa mazingira ya sasa , bila wapinzani kuungana hawataweza ku-survive maana ni wazi kuna mkakati wa kuua upinzani, na ndani ya wapinzani kuna vibaraka wengi ambao sasa wanarudi CCM na kutoa fursa kwa wapinzani kubakiwa na wapinzani halisi ambao itawapasa kuunganisha nguvu ili waweze kupambana na dola na CCM.

Kwa maana hiyo, kuna uwezekano wa asilimia 75 kwa Maalim na wenzake kujiunga na Chadema ili waweze kusimama Zanzibar, ukizingatia kuwa Chadema haina msingi imara Zanzibar.

Kama upo mkakati wa makusudi kuisambaratisha CUF kutoka kwa dola na CCM, bila shaka watajuta sana iwapo Maalim na kundi lake wataenda Chadema. Ikumbukwe kuwa kwa siasa za Zanzibar, vyama vilivyopo ni kivuli cha vyama vikivyokuwepo kabla ya Mapinduzi ya 1964; ASP, ZPP, na ZNP, ni vyama vilevile vyenye majina mapya.

Vv
 
Nadhani endapo Maalim Seif atahamia CDM basi naamini mpasuko mkubwa sana utakuwa ndani ya CDM kwanin nasema hivi chadema haijawa well organized hasa visiwani sasa kumleta Seif nadhani haitokuwa na tija sana huku bara na hata visiwani. Maalim atulie siasa ya bongo haiwezi kubadilika kwa maana mwenye maamuzi anaamua bila kujali matokeo yakoje.
Kwa yako taarifa tu Maalim akiingia CDM ni kihoro kwa CCM na CUF lipumba.
Na tunaposema maalim tunamaanisha pamoja na watu wanomuamini ikiwemo majority ya wawakilishi na wabunge wake na kwa uhuru wa Zanzibar ulkuhusu malumbano ya kisisa CDM wakipata jukwaa hilo kupitia CDM Maalim hakika CCM zenji na CCM magogoni watapata taabu sana
 
Maalim na watu wake wa Zanzibar wakihamia CHADEMA ni pigo kuu Takatifu kwa CCM maana misheni yao ya kuiua CUTF Zanzibar itafeli vibaya mno. Just imagine muungano wa CUF na CHADEMA via UKAWA ulivyoifanya Maalim na CUF yake kuishinda CCM kwa gapu kubwa sana haijawai kushinda kiasi hicho. Sasa fikiria Combination hiyo ndani ya Chama kimoja. Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu Maalim Seif, Mkamo mwenyekiti Juma Duni au Jussa hatari sana
 
Nadhani endapo Maalim Seif atahamia CDM basi naamini mpasuko mkubwa sana utakuwa ndani ya CDM kwanin nasema hivi chadema haijawa well organized hasa visiwani sasa kumleta Seif nadhani haitokuwa na tija sana huku bara na hata visiwani. Maalim atulie siasa ya bongo haiwezi kubadilika kwa maana mwenye maamuzi anaamua bila kujali matokeo yakoje.
huijui historia ya visiwani wewe . wale sio kama nyinyi mikia huku. kule ni zaidi ya chama cha siasa. wakisema hapana hapana tangu karume ipo hivyo. soma vizur historia ya vile visiwa
 
Nadhani endapo Maalim Seif atahamia CDM basi naamini mpasuko mkubwa sana utakuwa ndani ya CDM kwanin nasema hivi chadema haijawa well organized hasa visiwani sasa kumleta Seif nadhani haitokuwa na tija sana huku bara na hata visiwani. Maalim atulie siasa ya bongo haiwezi kubadilika kwa maana mwenye maamuzi anaamua bila kujali matokeo yakoje.
Ukawa ilikuwa ikiunda vyama vingapi?
 
Sakaya hahakosea kuwa cdm wanamtaka Maalim ili wajiimarishe tu. Mana zenj hawana ushawishi. Ushauri ni maalim kuanzisha chama kipya akiona Cuf hakuna liwalo
 
Julius Mtatiro ana siri nyingi sana za Maalim hata yule mganga wake ambae humsafishiaga nyota huko ungazija Komoro ameshajulikana .

Hapa ndio Mtatiro anapoingia ulingoni maalim anaweza asifikie uamuzi kwa sababu ya ulimi na mikono kuvimba.
 
Wabunge Znz wataongezeka na ruzuku itakua ya kutosha upande wa chadema ahame haraka
 
Nadhani endapo Maalim Seif atahamia CDM basi naamini mpasuko mkubwa sana utakuwa ndani ya CDM kwanin nasema hivi chadema haijawa well organized hasa visiwani sasa kumleta Seif nadhani haitokuwa na tija sana huku bara na hata visiwani. Maalim atulie siasa ya bongo haiwezi kubadilika kwa maana mwenye maamuzi anaamua bila kujali matokeo yakoje.
Hatutaki ushauri wenu nyie watu wa CCM.
 
Back
Top Bottom