Maalim seif mbona kimya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Mara baada ya kuukwaa uheshimiwa sijamsikia tena maalimu SEIF wa Zanzibar... kakaa kimya kama hayupo vile...ile misimamo yake ya kumbozi imeishia wapi kwa huyu bwana mkubwa?? au na yeye keshachukua chake anasubiri kustaafu kwa heshima na kula mema ya nchi...

Kuna tetesi nyingi nazisikia kupitia vyombo vya habri kuhusu huyu mheshimiwa lakini sijui kama ni za kweli

1)Hali yake ya kiafya sio nzuri hivyo hutumia muda mwingi hutumia kupaa na madege kwenda kutibiwa ulaya..
2)Nyingine ni kuwa wameamua kukubaliana ka CCM kutoumbuana hadharani ili ndoa yao idumu hali iliyopelekea kuufyata mkia
3)Hana mpango wa kugombea tena nyadhifa za juu serikalini hivyo hana cha kupoteza

Hivi tatizo la viongozi wetu hasa wanaoonekana kutupigania wanyonge kwa moyo mmoja huwa ni kuukwaa tu uheshimiwa ili wachumie matumbo na kuandika historia??
ni maoni yangu tu
 
Hujui kuwa madaraka ndiyo kipimo cha tabia ya mtu?. Kabla ya madaraka alikuwa ameficha tabia yake na akajionyesha kuwa mtetezi wa wanyonge, lakini madaraka yamemwonyesha hasa alivyokuwa. Na itakuwa hivyohivyo kwa chadema wakifanikiwa kuchukua nchi.
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
 
Back
Top Bottom