Jana Maalim Seif, makamu wa kwanza wa rais SMZ, alitua Mwanza airport na kusababisha kama kawaida adha kubwa kwa watumiaji wengine wa barabara, baada ya vipenyo na barabara zote alizopanga kupitia kufungwa ili yeye apite kwa amani na kwa heshima kubwa kama kiongozi.
Alitokea airport, akaenda kupata lunch Gold Crest Hotel, akaenda kwa Kabwe Wilson ofisi za jijini na baadae kuelekea wilayani Kwimba.
Masuala ninayojiuliza ni haya:
(a) Maalim Seif, ana wajibu kikatiba wa kufanya ziara jijini Mwanza ikizingatiwa yeye ni kiongozi wa SMZ?
(b) Na kwimba alienda kufanya nini?
Hapana mkurupuko huu lazima kuna mtimua nyongo hukokwenye serikali ya Umoja wa Zanzibar na pengine jambo zito zaidi liko nyuma ya mzani wa kupimia nyama kwa namna ambavyo sisi wanunuzi wa ujumbe anaotembeza hivi sasa kamwe halijawa wazi kwetu.
Ndevu hana lolote yote hiyo ni katika harakati za kumshughulikia Mpiganaji HAMAD RASHID..ikulu ya zanzibar sasa haikaliki tena mpaka HAMAD RASHID akione cha moto,mbaya zaidi ni tax payers money ndio inayotumika!
Kwimba kuna mganga mashuhuri mpaka kajengewa nyumba na serikali, Kikwete kila mara lazima aende kuhiji pale
seif mpemba hawezi kufuata uganga kwimba....akauacha mwambe na bumbwini...!yuko katika ziara za 'kuimarisha uhai" wa chama tu
polisi wako tayari kuongoza msafara, vingo'ora vinalia, barabara zimefungwa
Hivi kwanini JK huyu anaendelea kuvunja katiba ya JMT ambayo aliapa kuilinda? Mbaya zaidi na sisi Mi-Tanganyika
tupo tu kimya tunamkenulia meno bila kuchukula hatua.