Maalim Seif: Bado niko hai.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif: Bado niko hai..

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akiwa amelazwa katika hospitali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam jana. Seif amelazwa hospitali hapo tangu Ijumaa akisumbuliwa na ugonjwa wa mkamba.

  HALI ya tashwishwi ilikuwa imelipata Jiji la Dar es salaam na visiwa vya Zanzibar jana asubuhi baada ya uvumi kuenea kwa kasi ukieleza kuwa katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad amefariki na kumlazimu mwanasiasa huyo mkongwe ajitokeze na kusema: ""Jamani mimi sijafa".

  Kuanzia Ijumaa katibu huyo wa CUF alikuwa amelazwa Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam ambako alilazimika kuzungumzia afya yake mbele ya waandishi wa habari.

  "Jamani mimi sijafa, ninaendelea vizuri na huenda kesho (leo) nikaruhusiwa kurudi nyumbani," alisema Maalim Seif ambaye aliripotiwa kuugua ghafla akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam akijiandaa kusafiri kwenda Muscat, Oman.

  Uvumi wa kifo cha Seif ulisambaa jana jijini Dar es Salaam na Zanzibar ambako wafuasi wapenzi wa CUF na Watanzania wengine walionekana kukaa katika makundi wakitafakari taarifa hizo.

  Simu kadhaa zilipigwa kwenye ofisi ya gazeti la Mwananchi kutaka uhakika wa habari hizo za kustua ambazo ziliifanya CUF ililazimike kutoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kufafanua kuhusu habari hizo.

  Uvumi huo ulichochewa zaidi na usiri uliojitokeza awali katika kupata taarifa za afya ya kiongozi huyo baada ya magazeti kuripoti kuwa aliugua ghafla akiwa uwanja wa ndege. Madaktari wa Hindu Mandal walikataa kusema lolote wala kuwaruhusu waandishi kumwona Seif.

  Kutokana na uvumi wa kifo chake kusambaa kwa kasi, wasaidizi wa Maalim Seif walilazimika kuwaruhusu waandishi wa habari kumwona kiongozi huyo wa upinzani visiwani Zanzibar ambaye naye alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi huo.

  "Namshukuru Mungu kwamba naendelea vizuri, tofauti na nilivyofika hapa, nimepata huduma hali yangu inaendelea vizuri," alieleza Maalim Seif alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika chumba alicholazwa.

  Kauli hiyo ya Seif iliungwa mkono na Dk Kaushiki Ramaiya wa Hindu Mandal ambaye aliwaambia waandishi kuwa hali ya kiongozi huyo inaendelea vizuri na kwamba huenda leo atatoka hospitali.

  "Maalim Seif anaendelea vizuri, nimetoka kumuona asubuhi hii (jana) kwa kweli anaendelea vizuri tofauti na hali aliyokunayo siku ya Ijumaa ya Machi 5," alisema Dk Kaushik.

  Aliongeza kusema:"Nitakwenda kumuona tena kesho (leo) asubuhi na kama hali itakuwa nzuri zaidi, basi nitamruhusu kwenda nyumbani."

  Dk Kaushik alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kumpatia vipimo walimshauri kupumzika hapo kwa siku tatu hadi nne.

  "Kinachomsumbua ni siri ya daktari na mgonjwa mwenyewe kwa hiyo mimi siwezi kuwaambia, lakini Maalim Seif alifikishwa hapa Ijumaa tukamfanyia vipimo na kumpumzisha," alisema Dk Kaushik.

  Lakini kurugenzi ya habari na mahusiano na umma ya CUF ililazimika kuvunja ukimya kwa kueleza kinachomsumbua kiongozi huyo kuwa ni ugonjwa wa mkamba (bronchitis), ugonjwa ambao hutokana na kuvimba kwa njia za hewa baada ya mapafu kushambuliwa na vijidudu.

  Mkurugenzi wa idara hiyo, Salim Bimani alisema katika taarifa hiyo kuwa "Maalim Seif hajafa na anaendelea vizuri katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam na kwamba taarifa za uvumi kuwa amefariki si za kweli".

  "Daktari wake amejiridhisha kwamba maalim Seif ataweza kuendelea na shughuli zake za kawaida katika siku chache zijazo," inasisitiza taarifa hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo Seif alikuwa akisumbuliwa na tatizo hilo kwa siku kadhaa lakini, alikuwa akiendelea vyema na shughuli zake hadi alipokutwa na tatizo hilo wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema tatizo la Maalim Seif ni la kawaida na kwamba tiba yake ni kupata utulivu tu.

  Alisema walikubaliana baada ya kwenda kumuona juzi kuwa aendelee kupumzika hospitalini hapo kwa kuwa akienda nyumbani msongamano wa watu kwenda kumuona utakuwa mkubwa, jambo ambalo lingemchelewesha kupona haraka.

  "Mimi nilienda jana (juzi) kumwona na tukakubaliana asirudi nyumbani kwanza, kwa kuwa anahitaji kupumzika hii ndiyo tiba yake. Sasa ukimpeleka nyumbani hatapata muda wa kupumzika," alisema Profesa Lipumba.

  Mwananchi ilikuwa ikipokea simu nyingi kutoka bara na visiwani zikitaka kujua ukweli wa taarifa za kifo cha Maalim Seif, baada ya kusambaa kwa uvumi kwamba amefariki dunia.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  JAMANI NINGALI HAI!

  photos [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  Majira ya mchana LEO, uvumi ulienea katika jiji la Dar es salaam kama moto wa petroli eti maalim Seif kafariki dunia!!! kama inavyojulikana Dar kwa umbea, hali hiyo ilisababisha watu kuanza kupigiana simu na kutumiana meseji kueneza kifo hicho cha uzushi. Kiukweli Maalim yu ngali mzima ingawa kweli alikimbizwa hospitali jana baada ya kupandwa presha na kisukari. Kamera yetu ilitia timu Hindu Mandal hospital ambako amelazwa na kuongea nae na kusema kuwa uvumi huo ameusikia lakini anamshukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri kama anavyoonekana akiwa katika kitanda chake na huenda akaruhusiwa kurejea nyumbani baadae leo!
   
Loading...