Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na aliekua balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Green.
Siku moja tu baada ya maalim na ujumbe wake kuwasili Marekani katika jiji la Washington DC wanaharakati na wanasiasa waliobobea katika ngani za “political science and democracy” wamesema wazi kuwa Seif Sharif Hamad hana “tendency and property” za Kiafrika wala Kiarabu katika fani ya siasa, hayo waliyasema alipokuwa akitambilishwa kwa baadhi ya wajumbe watakaoshiriki katika mazungumzo ya kujadili hali ya siasa Tanzania na ufutaji wa matokeo halali ya uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 ambapo Seif Sharif Hamad alishinda uchaguzi huo na NDI walishuhudia uchaguzi huo.
Maalim Seif alimfananishwa na Nelson Mandela wa South Africa, Shimon Perez wa Israel, Jimmy Carter wa marekani, na watu kama Kurlt Warldheim wa UN katibu mkuu wa zamani.
Wakasema angalia yatokeayo Burundi hivi sasa, Kenya, Uganda na kwengineko duniani lakini maalim bado kaweza ku-resist yeye binafsi na kuwatuliza watu wake bila ya kufanya vurugu na wakati huo huo wakitoa haki yao iliyoporwa ambayo inasindikizwa na nchi ya jirani Tanganyika.
Sisi NDI na CSIS tulioutisha mkutano huu tunalipongeza hilo na tunaomba watu wengine wenye migogoro ya aina hii waige mfano huu wa Seif Sharif Hamad na sisi tutakuwa pamoja nao mpaka haki intendeke na ipatikane tukianzia na zanzibar.
Maneno hayo yalisemwa na mmoja wa wakurugenzi wa NDI bwana Peter Craig katika hotel moja hapo Washington.