Maalim Seif akiri kufanyiwa hisani ya matibabu na viongozi wa CCM

1974hrs

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
741
536
Sarakasi za wanasiasa hizi!!!

=================

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa chama chake kususia uchaguzi wa marudio uliafikiwa na Baraza Kuu la Uongozi na hauna uhusiano na taarifa kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Seif amelazimika kutolea ufafanuzi ukarimu aliofanyiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumlipia safari ya matibabu kwenda India; Serikali ya Jamhuri ya Muungano kulipa gharama za kuwepo katika Hoteli ya Serena na kutembelewa na viongozi wa ngazi za juu akisema, havina uhusiano na kurubuniwa.

magu-na-seiff.jpg

Katika kile kinachoonekana ni ‘kuwaangukia’ wanachama wake kupitia mkutano wa waandishi wa habari aliofanya jana mjini hapa, Seif alisema huo ni ukarimu na utamaduni wa viongozi unaotokana na ubinadamu .

Alisema uamuzi wa kujitoa katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ulitokana na chama hicho kutokubaliana na uamuzi uglification na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa sababu uchaguzi huo ulikidhi mahitaji na matarajio ya wananchi CUF iwe madarakani.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CUF, zipo taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kwamba alijitoa kwenye uchaguzi huo wa marudio baada ya kurubuniwa na CCM ili ipate ushindi mkubwa.

“Taarifa hizo hazina harufu ya ukweli,” alisema. “Kilichofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kugharimia safari yangu ya kwenda India matibabuni pamoja na kutembelewa na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais John Magufuli , kwanza ni wajibu wa serikali kwa sababu mimi ni Makamo wa Kwanza wa Rais mstaafu….lakini huo ndio ukarimu na uhusiano wetu Watanzania unaotokana na ubinadamu,” alisema.

Chanzo: Mtembezi
 
alitibiwa kama makamu ya rais wa serikali ya umoja wa kitaifa na sio kukirimiwa.
acheni hadith
 
Mtahangaika sana kuhalalisha uporaji wa ushindi wa cuf zanzibar, bahati nzuri kila mtu duniani anafahamu kilichotokea
 
Hayo yashapita, sasa hivi tunataka kujua wezi wa yake mabilioni ya Polisi na NSSF.
pia hao wabunge majangili ni nani?
Mumezoea kutupoteza lengo kwa kuleta mijadala ya kimzahamzaha
 
Hata ww raia serikali yako ilitakiw ikupeleke india ukatibiwe km tz wakishindwa.
 
Mleta sijakuelewa unapesema sarakasi za wanasiasa hizo ni kodi zetu hamna mtu aliyetoa pesa yake mfukoni.
 
Sarakasi za wanasiasa hizi!!!

=================

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa chama chake kususia uchaguzi wa marudio uliafikiwa na Baraza Kuu la Uongozi na hauna uhusiano na taarifa kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Seif amelazimika kutolea ufafanuzi ukarimu aliofanyiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumlipia safari ya matibabu kwenda India; Serikali ya Jamhuri ya Muungano kulipa gharama za kuwepo katika Hoteli ya Serena na kutembelewa na viongozi wa ngazi za juu akisema, havina uhusiano na kurubuniwa.

View attachment 336465

Katika kile kinachoonekana ni ‘kuwaangukia’ wanachama wake kupitia mkutano wa waandishi wa habari aliofanya jana mjini hapa, Seif alisema huo ni ukarimu na utamaduni wa viongozi unaotokana na ubinadamu .

Alisema uamuzi wa kujitoa katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ulitokana na chama hicho kutokubaliana na uamuzi uglification na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa sababu uchaguzi huo ulikidhi mahitaji na matarajio ya wananchi CUF iwe madarakani.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia CUF, zipo taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kwamba alijitoa kwenye uchaguzi huo wa marudio baada ya kurubuniwa na CCM ili ipate ushindi mkubwa.

“Taarifa hizo hazina harufu ya ukweli,” alisema. “Kilichofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kugharimia safari yangu ya kwenda India matibabuni pamoja na kutembelewa na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais John Magufuli , kwanza ni wajibu wa serikali kwa sababu mimi ni Makamo wa Kwanza wa Rais mstaafu….lakini huo ndio ukarimu na uhusiano wetu Watanzania unaotokana na ubinadamu,” alisema.

Chanzo: Mtembezi
bagi tupu
 
Back
Top Bottom