Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,603
- 22,717
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema amepata moyo na kufarajika sana kuona vijana wa Zanzibar wana ari kubwa ya kutetea nchi yao kuliko ilivyo kwa wazee na kila siku zinavyo kwenda kasi ya vijana kudai mamlaka ya Zanzibar inazidi kuimarika.
Maalim Seif, aliyasema hayo hoteli ya Bwawani mjini hapa, alipokuwa akizungumza kwenye Kongamano lililojumuisha wawakilishi kutoka vyuo vikuu na taasisi za elimu ya Juu 13 zilizopo Zanzibar, lililojadili nafasi ya wasomi katika kuleta mabadiliko na maendeleo Zanzibar.
Maalim Seif, alisema historia inaonyesha harakati zinazosimamiwa na kuongozwa na vijana, mara zote hupata mafanikio makubwa na ndio maana hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliongoza vyema Tanu hadi kuleta Uhuru wakati huo ambako alikuwa ni kijana shababi.
Alieleza kuwa, mbali na Mwalimu, hata Waziri Mkuu Mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim, alipewa ubalozi nchini Misri na marehemu Mzee Karume akiwa na miaka 22 na alifanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa, mbali na yeye (Maalim Seif), pamoja na vijana wengine ndani ya CCM, ambao waliweza kukitikisa chama hicho na kuleta mabadiliko makubwa wakiwa vijana.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, alisema katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye kura ya maoni, pamoja na uchaguzi mkuu wa mwakani, vijana hawatakiwi kulala na wanahitajika kuungana na wote wanaoendesha kampeni ya hapana, kama vile UKAWA dhidi ya Katiba inayopendekezwa.
Aliwatanabaisha kuwa, kama wanataka mamlaka kamili ya Zanzibar, watambue Katiba inayopendekezwa inaitoa roho Zanzibar na kweli ni koti la Muungano linalozidi kuibana Zanzibar, hivyo ni vema kuungana pamoja kupiga kampeni ya hapana ili katiba hiyo isipate nafasi.
Katika risala yao iliyosomwa na mwanafunzi Hafidh Ali Hafidh, wanafunzi hao walisema walifarijika baada ya Rais Jakaya Kikwete kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba, lakini baadaye wamefadhaishwa na yaliyotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume na waliyoyataka wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema wao kama vijana, walipatwa na wasiwasi mkubwa baada ya kuona baadhi ya Wazanzibari waliokubali Serikali tatu Zanzibar, walipofika Dodoma wamebadilika na kufuata sera ya chama chao.
"Kitendo kilichofanywa na wana CCM hao ni uhalifu mkubwa na ni ubaguzi mkubwa ambao hatukubaliani nao na Katiba wanayoipendekeza haifai, hivyo tutakuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni ya ‘Hapana'" walisema katika risala hiyo.
Hafidh, alisema kwa Katiba inayopendekezwa, hatma ya Zanzibar imewekwa katika kuti kavu na sasa inadhihirika wazi, wapo baadhi ya watu wanataka Zanzibar ifutike kabisa katika ramani ya Dunia, jambo ambalo Wazanzibari wazalendo hawatalikubali.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, alisema wimbi la mabadiliko linaloikumba Zanzibar na Tanzania nzima, hakuna wa kulizuia na wala watu wasipite kuwadanganya wananchi.
Jusa ambaye pia ni Mwakilishi wa CUF Jimbo la Mji Mkongwe, alisema Wazanzibari walio wengi walidhani viongozi wa CCM watakubali kuleta mabadiliko kwa njia za kistaarabu baada ya wananchi kutoa maoni yao na kuratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini ni kinyume chake kwa vile wameyapiga teke maoni hayo.
Chanzo: Tanzania Daima