Maajabu ya Tanzania hayatakwisha!!!!

MANILABHONA

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
462
350
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni.
Kigogo mmoja mkuu wa Idara fulani ya Afya huko Kigoma amehamishiwa mkoani Mwanza baada ya hali kuonekana si shwari hapo, hasa baada ya kuthibitika kuwa alitumia lugha ya kudhalilisha kwa watumishi walio chini yake na kesi hiyo kufikishwa mahakama ya usuluhishi ambapo alipewa hukumu na hukumu hiyo kupelekwa kwa msimamizi wake wa kazi, baadae bado aliendelea kuwadhalilisha watumishi hao hasa mabinti wa kike(wauguzi) kingono hadi hapo mke wake alipoamua kumng'ata meno mmoja wa watumishi mabinti hao.

Naona hii ilimalizwa kimyakimya na msimamizi wake wa kazi. Cha ajabu sasa ni utaratibu wa uteuzi kwa viongozi kutokufuatwa.

Inawezekana vipi kwa kiongozi asiye na maadili kwa kiasi hiki badala ya kuchukuliwa hatua zinazostahili anahamishwa aende kuendeleza ufedhuli huo sehemu nyingine. Magufuli angalia vizuri walio chini yako wanakusaliti!!!!!
 
Back
Top Bottom