๐— ๐—ฎ๐—ฎ๐—ท๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฃ๐—ฟ๐—ผ๐—ด๐—ฟ๐—ฎ๐—บ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฆ๐—ถ๐—บ ๐—ง๐—ผ๐—ผ๐—น๐—ธ๐—ถ๐˜ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐˜‡๐˜„๐—ฎ!!!

๐— ๐—ฎ๐—ฎ๐—ท๐—ฎ๐—ฏ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฃ๐—ฟ๐—ผ๐—ด๐—ฟ๐—ฎ๐—บ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฆ๐—ถ๐—บ ๐—ง๐—ผ๐—ผ๐—น๐—ธ๐—ถ๐˜ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐˜‡๐˜„๐—ฎ!!!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
1_20250602_152225_0000.png


Kuna app iko kwenye kila simu unayoijua wewe hapa Duniani, lakini watu wengi hawaijui vizuri na hawajawahi kuijaribu kuitumia Hata mara moja wengi wanaiogopa kabisa.

Unajua kwanini!!!๐Ÿƒ๐Ÿƒ Je app hii inafanya kazi gani ? Kwanini ipo kwenye kila simu ?? Leo nitakujuza kabisa๐Ÿ˜‹.

2_20250602_152225_0001.png


Sim Toolkit ni app ambayo inapatikana kwenye simu yako ambayo inakuja na kila line ya simu unayoweka kwenye simu yako ili kupiga simu na kutumia data.
Program hii mara nyingi hufupishwa kuwa STK utakutana nazo kwenye simu nyingi za Android.

Sim Toolkit inaunganisha simu yako na mtandao wa simu ( Airtel,Tigo, Vodacom,halotel,Ttcl au nyinginezo). Sim Toolkit inakusaidia kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi kupitia simu yako kuanzia;

3_20250602_152225_0002.png


โšก Kununua bando
โšก Kutuma salio
โšก Kubadilisha pin
โšก Masuala ya kifedha
โšก Kujiunga na promosheni mbalimbali nk.

Kila unachokifanya kwenye hii app ni Amri yako haiwezi kufanya chochote bila amri yako hivyo usijali kabisa haiwezi kusoma sms yako yoyote, kuchukua taarifa za app zinginezo nk.

4_20250602_152225_0003.png


Kubwa zaidi inafanya kazi bila mtandao (intaneti) kwani yenyewe inatumia USSD (unstructured supplimentary services data), unaweza nunua bando bila kuandika zile code za kununua bando.

5_20250602_152225_0004.png
6_20250602_152225_0005.png


Unaweza lipia bili, kutuma pesa, kununua kifurushi, kufuatilia Matumizi mbalimbali ya simu yako bila kuhitaji app kama vile mix by yas , Airtel app, m pesa nk.

7_20250602_152225_0006.png


Umeshawahi kutumia hii app ya STK kwenye simu yako au ulikua
unashangaa tu ??
 
Asante sana kwa elimu, sikuwahi kufikiri hili, nimeangalia, ulichosema ni kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom