lackg
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 641
- 268
Katika vitu vilivyonishangaza mwaka huu ni hili la rafiki yangu Polepole. Kuna jambo linafanana sana ila lina majina tofauti, Polepole ni katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM, chama kinachojipambanua na kujiita CCM mpya ( weka moja kichwani) Na Nape alikuwa na wadhifa huohuo kabla na baada ya uchaguzi 2015 na juzi amesema alipambana kuitoa CCM shimoni (weka moja kichwani)
Sasa Polepole anasema kitendo cha Nape kuiita CCM ilikuwa shimoni ni utavu wa nidhamu na anapaswa ajieleze kwenye kamati ya Mangula. Lakini Polepole na mwenyekiti wake wa sasa wanasahau kuwa wao wanaiita hii CCM mpya kwa tafsiri ya harakaharaka CCM ya zamani;
(a)ilikuwa imechoka
(b)ilikuwa imechakaa
(c)ilikuwa imepoteza dira na mvuto kwa wananchi
(d)ilikuwa shimoni, au
(e)a, b, c na d zote ni sawa!
Sasa tofauti ya kauli ya Nape na Mtazamo wa Polepole kuhusu CCM ya zamani na ya sasa ni ipi?!?
...... Karibini wadau tujadili....