Waziri aishukia DAWASCO
*Akana kudaiwa ankara
*Asema DAWASCO inaingiza hasara
Na Said Mwishehe
MVUTANO wa chini kwa chini unaoonekana kujitokeza tangu Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) lilipoelezwa kutangaza operesheni maalum ya kuwakatia maji vigogo wanaodaiwa na shirika hilo,zikiwemo wizara kadhaa, jana ulionekana kuingia katika sura yingine baada ya Waziri wa Maji, Bw. Shukuru Kawambwa kukanusha taarifa kuwa anadaiwa na pia kuwatetea mawaziri wengine.
Jana Waziri Kawambwa alivunja ukimya dhidi ya shutuma hizo kwa kusema yeye hadaiwi huku akisisitiza hata mawaziri wanaoishi eneo la Masaki, Dar es Salaam hawakukatiwa maji, kama ilivyowahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Juzi akizungumza na vyombo vya habari, Ofisa Mtendaji mKUU wa DAWASCO, Mhandisi Alex Kaaya alisema wao hawakutaja kuwa mawaziri wanadaiwa bali walitaja maeneo yanayodaiwa. Masaki ni moja ya maeneo yaliyotajwa na ndiko wanakoishi vigogo wengi.
"Kama Waziri wa Maji sidaiwi na DAWASCO, nimekuwa nikifanya kazi kwa maadili na ninaheshimu sera za maji," alisisitiza Dkt. Kawambwa.
Alisema anafahumu DAWASCO inajiendesha kwa kutegemea fedha za wateja wake hivyo kila mtu anawajibu wa kulipa bila ya kusubiri kusukumwa na yeye amekuwa akifanya hivyo na wala hatarajii kuwa mdaiwa wa DAWASCO.
Kuhusu mawaziri kudaiwa kukatiwa maji wakiwa miongoni mwa wadaiwa sugu, Dkt. Kawambwa alisema: "Naomba niseme kuwa hakuna waziri ambaye amekatiwa maji na DAWASCO katika eneo la Masaki wakati ilipokuwa ikifanya operesheni ya kuwakatia huduma ya maji wadaiwa sugu kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
"Hata hivyo sina maana kuwa hakuna waziri anayedaiwa maji inawezekana wapo kwani nao ni sehemu ya wateja wa DAWASCO na kwa mujibu wa Sera kama wapo wanatakiwa kulipa."
Kupitia mkutano huo Dkt. Kawambwa aliweka hadharani kuwa DAWASCO imekuwa ikijiendesha kwa hasara.
Alisema Serikali ndiyo inabeba mzigo mzito kwa kutoa sh. milioni 600 kila mwezi ili kuweza kulisaidia shirika hilo kujiendesha.
Alisema kuwa takwimu zinaonesha kuanzia Julai hadi Novemba mwaka huu makusanyo ya DAWASCO ni sh. bilioni 1.6 wakati uendeshaji wake unafikia sh. bilioni 2.2 kiasi cha kuilazimu Serikali kutoa sh. milioni 600 ili kufidia mapungufu hayo.
"Serikali inabeba mzigo kwa kuiongezea DAWASCO milioni 600 kwa mwezi na hiyo inatokana na wakazi wa Dar es Salaam kuwa wagumu kulipa ukilinganisha na miji mingine kama ya Dodoma na Tanga. Nadhani si jambo zuri kuwa na huduma mbaya ya maji kwa watu kushindwa kulipa ankara za maji," alisema Dkt.Kawambwa.
Hata hivyo alisisitiza kuwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2007/2008 imechangia sh. bilioni 2 ili kuijengea uwezo DAWASCO iweze kuboresha utoaji huduma.
Aliwapa changamoto wananchi wa Dar es Salaam kubadilika na kulipa huduma wanazopewa ili zifikie kiasi cha kutosheleza gharama za uendeshaji ili huduma hiyo iweze kuboreshwa na kufikia wananchi wengi.
Aliahidi kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2008 huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam itakuwa imeboreshwa kwani utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa miundombinu ya utoaji wa maji safi na maji taka utakuwa umekamilika. Mradi huo utagharimu dola 164 ambazo ni fedha za mkopo kutoka kwa wahisani wakiwemo Benki ya Dunia.
"Naomba wateja walipe ankara zao kwa wakati ili kuondokana na usumbufu unaojitokeza na tutaendelea kukata maji kwa wadaiwa sugu lakini wale ambao hawadaiwi na kwa bahati mbaya wakakatiwa maji nawaomba radhi kwa makosa yaliyojitokeza na ninaamini DAWASCO itafanya kazi kwa umakini ili kuondoa tofauti zilizopo," alisema.
Tangu DAWASCO ilipotangaza 'vita' ya kuwabana wadaiwa sugu zikiwemo wizara kadhaa za Serikali, kumekuwa na sintofahamu ya chini kwa chini huku ikielezwa baadhi wa watendaji wakuu kwenye Wizara ya Maji hawakufurahishwa na kitendo cha kudaiwa kuwa mawaziri wanadaiwa.
DAWASCO imekuwa ikisisitiza kuwa ilitaja maeneo yenye wadaiwa sugu na haikutaja jina la mtu wala cheo chake.
Source: Majira