Maajabu ya karafuu

Maajabu ya karafuu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
MAAJABU YA KARAFUU (SYZYGIUM AROMATICUM) KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI.

attachment.php
karafuu.jpg
Unga wa karafuu.jpg

Karafuu pamoja na Unga wa karafuu

Karafuu ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10 hadi 12.
Karafuu imekuwa ikitumiwa India na Uchina kwa zaidi ya kwa zaidi ya miaka 2000 kama kiungo cha kulinda kuoza meno na kutoa harufu mbaya yaaani pumzi mbaya.

Mti wa karafuu una asili ya visiwa vya Molluca. Wachina walipata kiungo hiki mnamo karne ya 3 K.K (Kabla ya Kuzaliwa Kristo).
Karafuu ziliingizwa Alexandria mapema mwaka 176 B.K (Baada ya Kuzaliwa Kristo). Mnamo karne ya 4 hivi B.K ulijulikana vema katika meditarrania na katika karne ya 8 ulaya nzima.

Inasemekana huko visiwa vya pemba na unguja (Zanzibar) karafuu ililetwa na sultani mmoja ikiwa imewekwa kwenye fimbo ya mwanzi leo hii Zanzibar ndio mzalishaji anayeongoza kwa kuzalisha karafuu nyingi ulimwenguni.
Sifa ilizonazo karafuu ni wanga (carbohydrates), Protini, mafuta (Volatile oil), nyuzinyuzi (crude fibre), jivu la hydrochloric acid, calcium, phosphorus, iron, sodium,

Potassium, thiamine (Vit B1), Riboflavin (Vit B2), Niacin (Vitamin B3), vitamin A na C.
Mafuta hupatikana kwenye vitumba vya karafuu, kikonyo na majani.
Karafuu hutibu magonjwa mengi kama kutuliza maumivu ya meno, kutoa gesi tumboni, kuchafuliwa moyo, kuyeyusha chakula tumboni, kuimarisha viungo vya kiume (Sex Stimulant), kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, kuzuia kutapika,

Kipindupindu, kikohozi, Asthma, Masikio, maumivu ya Misuli (Muscular Cramps), kuumwa kichwa, styes (an inflammation around the eyelash).
Matumizi mengine ya karafuu huchanganywa kwenye curry powder, pilipili, mdalasini,

Binzari na viungo vingine. Wahindi hutumia kuongeza ladha kwenye betel quid (pan pati). Mafuta ya Karafuu pia hutumika katika viwanda ya perfume, sabuni, ni kuongeza ladha kwenye madawa n.k

Tunashauri kila familia kuzingatia matumizi ya karafuu ili kulinda afya zetu.

Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,

Vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.
 
MziziMkavu

...maelezo yako mbona ni ya jumla jumla sana!?,hakuna sehem hata moja umeeleza ni kwa kiasi gani Karafuu inaitajika kwaajili ya kutibu ugonjwa na inatumikaje...habari nzima inaonekana ni nzuri lakini haimwongezei msomaji maarifa kwani mwandishi haujasema mtu anaweza kuitimuaje Karafuu kama dawa...
 
Last edited by a moderator:

Maelezo mkuu namna gani tutumie karafuu twasubiri
 
Twanga karafuu upate kijiko 1 tia kwenye uji au maji ya uvuguvugu kunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 au siku 7 pia waweza kuchanganya karafuu na Asali kwa ajili ya dawa ya kuongeza nguvu za kiume kazi kwenu.
 
jaman hiv kila kitu siku hizi dawa ya nguvu za kiume,bado kidogo tutaambiwa mavi pia ni dawa,
 
Twanga karafuu upate kijiko 1 tia kwenye uji au maji ya uvuguvugu kunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 au siku 7 pia waweza kuchanganya karafuu na Asali kwa ajili ya dawa ya kuongeza nguvu za kiume kazi kwenu.

Asante
 
MziziMkavu tumbo la hedhi karafu inatumikaje kulitibu
Usitumie Karafuu kwa ajili ya kutibu hedhi tumia dawa hizi hapa chini chaguwa una matatizo gani kuhus hiyo hedhi yako?

MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja

hata hivyo nayo yana tiba yake inayolingana na aina ya tatizo husika.

TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA)
: Kanuni ya kwanza: Tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka hedhi. Dawa hii ni hatari kwa mwanamke mja mzito, hivyo atahadhari nayo,na tangu hapoyeye haimuhusu.

Kanuni ya pili: Chukua Harmal gramu 50, uchemshe ndani ya maji lita moja. Ikishapoa uichuje. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara mbili kwa muda wa siku tatu.

TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI:
Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu.

TIBA YA HEDHI INAYOTOKA KWA WINGI ZAIDI YA ADA:

TIBA Kanuni ya kwanza
Chukua kijiko kimoja cha maua ya Babunaji (Chamomile) ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Yakishapoa, unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu kabla ya kula.

Kanuni ya pili:
Chukua zaatar kijiko kimoja kikubwa cha chakula ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Kunywa kikombe cha chai kutwa mara tatu.

TIBA YA MAUMIVU YA HEDHI YANAYOTOKA KIDOGOKIDOGO (DYSMENORRHOEA):
Kanuni ya kwanza: Chukua nanaa na utayarishe mfano wa chai. Kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu.

Kanuni ya pili:
Chukua mvuje wa kidonge (kidonge kimoja ) na unga wa pilipili manga (black Peper) gramu 50. Weka dawa hizi mbili ndani ya glasi moja ya maji kisha uifunike na uiache ilowane. Bila ya kuchuja kunywa kijiko kimoja kikubwa kutwa mara moja .Rudia tena kunywa siku ya pili ikiwa hujapata mabadiliko.Dawa hii huzibua hedhi iliyoganda au kufunga.

TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA:
Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.
 
Naomba kujua jinsi ya kutumia kwa watu wanaoumwa ugonjwa wa asthma problem

attachment.php
​
attachment.php

Karafuu pamoja na Unga wa karafuu

Karafuu ni tumba lililokauka la maua yasiyofunguka yanayopatikana kutoka mti mzuri wa kati na kijani. Mti huu una shina lilinyooka na hukua kufikia kimo cha mita 10 hadi 12.
Karafuu imekuwa ikitumiwa India na Uchina kwa zaidi ya kwa zaidi ya miaka 2000 kama kiungo cha kulinda kuoza meno na kutoa harufu mbaya yaaani pumzi mbaya.

Mti wa karafuu una asili ya visiwa vya Molluca. Wachina walipata kiungo hiki mnamo karne ya 3 K.K (Kabla ya Kuzaliwa Kristo).
Karafuu ziliingizwa Alexandria mapema mwaka 176 B.K (Baada ya Kuzaliwa Kristo). Mnamo karne ya 4 hivi B.K ulijulikana vema katika meditarrania na katika karne ya 8 ulaya nzima.

Inasemekana huko visiwa vya pemba na unguja (Zanzibar) karafuu ililetwa na sultani mmoja ikiwa imewekwa kwenye fimbo ya mwanzi leo hii Zanzibar ndio mzalishaji anayeongoza kwa kuzalisha karafuu nyingi ulimwenguni.
Sifa ilizonazo karafuu ni wanga (carbohydrates), Protini, mafuta (Volatile oil), nyuzinyuzi (crude fibre), jivu la hydrochloric acid, calcium, phosphorus, iron, sodium,

Potassium, thiamine (Vit B1), Riboflavin (Vit B2), Niacin (Vitamin B3), vitamin A na C.
Mafuta hupatikana kwenye vitumba vya karafuu, kikonyo na majani.
Karafuu hutibu magonjwa mengi kama kutuliza maumivu ya meno, kutoa gesi tumboni, kuchafuliwa moyo, kuyeyusha chakula tumboni, kuimarisha viungo vya kiume (Sex Stimulant), kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, kuzuia kutapika,

Kipindupindu, kikohozi, Asthma, Masikio, maumivu ya Misuli (Muscular Cramps), kuumwa kichwa, styes (an inflammation around the eyelash).
Matumizi mengine ya karafuu huchanganywa kwenye curry powder, pilipili, mdalasini,

Binzari na viungo vingine. Wahindi hutumia kuongeza ladha kwenye betel quid (pan pati). Mafuta ya Karafuu pia hutumika katika viwanda ya perfume, sabuni, ni kuongeza ladha kwenye madawa n.k

Tunashauri kila familia kuzingatia matumizi ya karafuu ili kulinda afya zetu.

Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea), kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (Menorrhagia), kukawia kuingia hedhini (Amenorrhea), matatizo ya kukoma kwa hedhi (Menopause), kulegea kwa uzazi (vagina discharge), miguu kuwaka moto,

Vidonda vya tumbo, kufunga kuharisha, matatizo ya uvimbe wa kizazi na mengine mengi ambayo si rahisi kuyaorodhesha isipokuwa baadhi.
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua Tatizo analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi.[/QUOTE]
Naomba
 
Twanga karafuu upate kijiko 1 tia kwenye uji au maji ya uvuguvugu kunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 au siku 7 pia waweza kuchanganya karafuu na Asali kwa ajili ya dawa ya kuongeza nguvu za kiume kazi kwenu.

Mzizimkavu nimekumiss ukipatikana uje unitafutie dawa ya ......(...) nitakuinbox
 
Usitumie Karafuu kwa ajili ya kutibu hedhi tumia dawa hizi hapa chini chaguwa una matatizo gani kuhus hiyo hedhi yako?

MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja...

Mkuu kuhusu tatizo la Maumivu makali ya hedhi msaada naomba
 
Twanga karafuu upate kijiko 1 tia kwenye uji au maji ya uvuguvugu kunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 au siku 7 pia waweza kuchanganya karafuu na Asali kwa ajili ya dawa ya kuongeza nguvu za kiume kazi kwenu.

Mkuu kijiko kipi? kidogo au kikubwa?
 
karafuu+mdalasini+ASALI =tiba dawa ya nguvu za kiume.

kuongeza urefu wa uume pilipili+chumv+ limao=juice yake huongeza urefu wa uume.

big up JF
Pilipili@kuongeza nguvu za kiume..!!!???
DON'T TRY THIS....Utajuta kuzaliwa!
 
Tupe hiyo tiba na sisi tuwadaidie wengine au sisi maana first lady kauficha bora mzizimkavu ungetujuza na sisi pia, asante

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom