Maajabu ya ELIMU : Elimu ya nasaba !

Maajabu ya ELIMU : Elimu ya nasaba !

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,352
Huu ni muendelezo katika hali ya kuzinduana na kukumbushana pia. Elimu tamu sana hasa ukiichukua kutoka kwa watu wake.

Hapa siizungumzii elimu ya vinasaba,la hasha hapa nazungumzia elimu ya utambuzi wa nasaba za watu,yaani kuzijua koo,vizazi na makabila ya watu.

Ile elimu ambayo ukimtajia mwenye elimu hiyo jina la ukoo wako,basi anakutajia takribani mababu zako wa tano nyuma pamoja na historia zao kwa ufupi.

Katika ulimwengu wa kielimu katika mataifa mengine wenzetu wamezithibiti elimu hizi na wanaendelea kurithisha elimu hizi vizazi na vizazi.

Sijui kwa hapa kwetu Tanzania kama elimu hii inafahamika,na kama inafahamika wahusika wanatumia mbinu gani kuihuisha elimu hii ?

Uzi huu umekusudia kuwaita wale wote wenye elimu hii,ili watupe muongozo katika kujifunza elimu hii adhimu,ili tuweze kudhibiti koo zetu na kuzijua vyema asili zetu.
 
Tatizo kubwa letu kizazi cha leo ni ile kujifanya wadijitari, hatutaki kuzungumza na wala hata kuzijua lugha zetu za kikabila.
 
Back
Top Bottom