Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 968
- 542
- Thread starter
-
- #21
ushahidi mwingine wa ni jinsi gani walivyoimasikinisha nchi hii.Kitu kimoja najiuliza mabadiliko gani wanayoyataka ccm yatokee kwa kuwaweka watu wale wale wenye mtazamo ule ule?Huu ni mzaha na kucheza na akili za watanzania.
hiyo ndo kiboko ya CHADEMA. wazee wenye busara wapo CCM, chadema kuna wazee hovyo wakiwakilishwa na Dr Slaa
yaelekea kwenu hakuna wazee. hayo uliyoandika sijui kama umeshirikisha ubongo wako
Nimeshangaa kuona Karume yumo kwenye list! Maana kila siku anatuhumiwa kushirikiana na watu wa "serikali ya mkataba"Hao wazee wa ccm wataitoa ccm toka kuvunda mpaka kuifanya ikawa ccm ilioza! Ccm hoyeee!
Hivi kuvuana magamba kuliishia wapi vile?Mbona nyie mmegeuka kuwa wasemaji wa CCM? ni hivi majuzi tu mlikuwa mnalalama kitendo cha HAMY-D kuweka hadharani uozo wa CHADEMA
Wanawapooza wazee baada ya Nape kusema wazee wanasubiri kufa.
Sasa hivi chama cha mapinduzi (CCM) kipo katika kikao maalum cha kamati kuu huko dodoma,pamoja na mambo mengine kinaandaa mabadiliko makubwa ya kichama na kuelekea katika mabadiliko hayo kamati ya wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu wameundiwa kamati maalum kusimamia mabadiliko hayo ya kichama. Miongoni mwa waliochaguliwa ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaji Ally H.Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu Benjamini mkapa,Pius Msekwa,Rais mstaafu wa Zanzibar Abeid Aman Karum nk.
Kitu kimoja najiuliza mabadiliko gani wanayoyataka ccm yatokee kwa kuwaweka watu wale wale wenye mtazamo ule ule?Huu ni mzaha na kucheza na akili za watanzania.