Maajabu ya bata

Clinker belite

Senior Member
Jan 19, 2020
116
1,000
Nipo kijijini kwetu one time.. hapa home kwa wazazi wanafuga bata miaka mingi saana. Sasa ile siku nafika toka town waliniambia nichinje bata kwa ajili yangu mgeni. Then nikichinja niwaite washughulikie.

Basi nkamchagua bata, nkamshika. Nkashika kisu nkawa natoka nae nkamchinje. Pale nje nikawa nakinoa kile kisu huku nmemshika bata. Then nkaenda nyuma ya nyumba nkamchinja yule bata.

Ebwana ile nyama baada ya kupikwa haikua nzuri kabisa.. yaan sio nzuri kama tulivozoea. Mama akanambia, wewe inaonekana huyu bata kabla hujamchinja, ulimuonesha kisu kwa muda mrefu. Na ni kweli nmenoa kisu, nmezunguka nae kumchinja huku nna kisu mkononi.

Maza akasema ungeandaa kisu kwanza ndo ukamshike. Bata akiona kisu na huku umemshika anaficha damu, so nyama yote huharibika. Nilishangaa sana.

Ajabu ya pili ya bata ambayo hadi leo huwa sielewi ni hii. Bata akiwa anataga mayai..huyahesabu.. ukiwa na tabia ya kuchukua mayai yake, kila akija akute yanapungua, hususa kutaga. Na hatagi kweli.. sasa me huwa najiuliza, mayai ya tumbon huyapeleka wapi?? Sababu nnachohisi mimi kutaga mayai sio tendo la hiyari. Ni lazima..ni mwili wenyewe.. yeye anaamuaje kuacha kutaga???

Kubwa kuliko, bata ukimuua ukianza kumnyonyoa manyoya, yanaota mengine.. mfano ukianza mgongoni kabla hujafika tumboni basi mgongoni utaona vimeanza kutoa.. yaani unaweza ukakesha kunyonyoa. Hii ya juzi maza alichofanya ananyonyoaa then anabanika, ili kuvikausha na hivi vidogo vinavoota upya
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,668
2,000
Hilo la kutaga sio mtaalamu sana.

Ila najiuliza,Mwanaume umedindisha kbsa muda wowote unaeza ukacheuwa wareno.
Unamwambia vua kyupi inatoka ng'onda ya hatari..daaah inatisha!

Au mdada unapeleka mdomo wako kwake unakutana na hewa nzito kuliko hewa ukaa..
Ivi ile ashiki inapoteleaga wapi.

Naona hakuna tofauti na bata aliyeibiwa mayai.
 

swahib sinjo

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
236
250
Hiyo ya kwanza ya kuficha damu na ya pili ya mayai sijui maana sijawahi kuifanyia uchunguzi ila ya tatu kuhusu manyoya sio kweli ni story za vijiweni tu, mara ukimnyonyoa huku unaongea yanaota tena sio kweli, kama week 2 zilizopita nilichinja bata na nimemnyonyoa peke yangu kwa muda mfupi tu huku story zikiendelea!!!!!
 

Clinker belite

Senior Member
Jan 19, 2020
116
1,000
Hiyo ya kwanza ya kuficha damu na ya pili ya mayai sijui maana sijawahi kuifanyia uchunguzi ila ya tatu kuhusu manyoya sio kweli ni story za vijiweni tu, mara ukimnyonyoa huku unaongea yanaota tena sio kweli, kama week 2 zilizopita nilichinja bata na nimemnyonyoa peke yangu kwa muda mfupi tu huku story zikiendelea!!!!!
Umri wake ulikua umeenda.

Ukimkamata bata ambae ni kinda.. utashuhudia.

Bata wazee hawaoti manyoya. Ndo maana wazee kijijini wana prefer kuchinja bata aliesogea umri.. ili kuepusha kero ya mayoya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom