PROFESA KYANDO
Member
- Jul 24, 2012
- 81
- 6
BAADA ya mapumziko ya miezi takribani mitatu, watunga sheria wamerudi tena bungeni kwa ajili ya kikao chao cha mwisho kwa mwaka huu. Waliondoka Dodoma mwezi Agosti baada ya kufanya vituko vingi vya kushangaza wakati wa kikao cha bajeti.
Baada ya maoni ya watu mbalimbali kuhusiana na jinsi walivyoendesha shughuli zao, ilidhaniwa kuwa safari hii watarudi wakiwa wamebadilika. Ilidhaniwa kuwa maoni hayo yangesaidia kuwapa mwanga zaidi wa nini jamii inatarajia kutoka kwao. Lakini hali ya mambo inaonesha kuwa hawajajifunza chochote.
Kwanza ni kwenye suala la utoro. Inashangaza na kusikitisha sana kuwa hata siku ya kwanza ya kikao wabunge walishindwa kuhudhuria kikao kiasi cha kumlazimisha spika kuahirisha kikao kwa sababu ya idadi ndogo ya wabunge waliokuwepo ukumbini.
Wabunge waliokuwapo ukumbini wakati hoja ya kujadili na hatimaye kupitisha au kutopitisha mkataba wa ushirikiano wa biashara baina ya Jumuiya ya Ulaya kwa upande mmoja, na nchi za Afrika, Pasifiki na Karibiani kwa upande mwingine, ilishindikana. Mkataba huu, ambao kwa kifupi unaitwa EPA, ni muhimu sana kwa masilahi si ya Tanzania tu, bali Afrika Mashariki kama jimbo na Afrika nzima kama bara.
Ni mkataba ambao unakusudia kutengeneza utaratibu wa kisheria na kikanuni kwa ajili ya kufanikisha biashara bila vikwazo baina ya maeneo hayo. Chini ya mkataba huo, nchi za Afrika zitakuwa na fursa ya kuuza bidhaa zao katika soko la Jumuiya ya Ulaya bila ya vikwazo vya kikodi. Wa Ulaya nao watakuwa na fursa kama hiyo iwapo watahitaji kuuza bidhaa zao Afrika.
Kwa muda mrefu kumekuwa na mijadala mizito kuhusu EPA. Wapo watu ambao wanaunga mkono mkataba huu wakiamini kuwa Tanzania na Afrika zitanufaika kwa sababu tutapata masoko ya uhakika wa bidhaa zetu. Lakini pia wapo wanaoupinga wakionya kuwa kwa hali jinsi ilivyo, Tanzania na Afrika hazijawa tayari kufanya biashara na nchi za Ulaya katika urari unaolingana.
Kwanza, wanasema, hatuna uwezo wa kuzalisha bidhaa za kutosheleza soko hilo kwa viwango ambavyo wao wameviweka. Kwa maana hiyo, kile tunachodhani sasa hivi kuwa ni fursa, itageuka kuwa ni dhahama kwetu kwa sababu hatutakuwa na cha kuuza pindi makubaliano haya yakiafikiwa na kuanza kutumika. Matokeo yake sisi tutageuka kuwa soko la bidhaa zao kwa sababu wao tayari wana vitu vya kuuza kwetu.
Ilitarajiwa kuwa wabunge wangeona umuhimu wa suala hili na kuhakikisha kuwa wanakuwepo ukumbini wakati wa kulijadili utakapowadia. Lakini kutokana na vituko vyao, wabunge wakaona kuwa jambo hilo si la maana wala la msingi, wakaamua kutokuja bungeni kulijadili.
Lakini ukiachilia mbali suala la kuacha kujadili jambo hilo, pia kuna suala la kujali muda. Hapa tatizo linaweza kuwa ni la kiutamaduni zaidi kuwa Watanzania bado hatuna mazoea ya kuuthaminisha muda. Katika karibu kila jambo kuchelewa kwetu si hoja kubwa sana ya msingi ya kumfanya mtu ashtuke.
Lakini kwa kufanya hivyo tunashindwa kufanya mambo mengi ya msingi na hii ni moja ya sababu kubwa inayotufanya tuwe nyuma kimaendeleo hadi hii leo. Watu wasiojali muda hawawezi hata kujali umaana wa jambo wanalopaswa kulifanya katika muda fulani, kama wabunge wetu walivyotuonesha.
Ajabu nyingine ambayo nimeishuhudia kutoka Bungeni ni uamuzi wa kutoiweka hadharani taarifa ya kamati ndogo iliyochunguza tuhuma dhidi ya wabunge kadhaa wa Kamati ya Nishati na Madini kuwa walijihusisha na rushwa. Inashangaza sana kuwa kwa wakati huu kiongozi wa taasisi nyeti kama Bunge anaweza kuwa na ujasiri wa kuzuia taarifa kama hiyo isiwekwe hadharani na kujadiliwa! Sijui ni ujasiri wa aina gani huu!
Hakuna asiyefahamu kuwa kama kuna jambo ambalo limepamba moto hivi sasa katika mizunguko ya kisiasa nchini ni rushwa. Nchi imenaswa katika utando wa rushwa kiasi kuwa watu wenye dhamira njema na nchi wangependa kuona kila jitihada inafanyika kuikwamua nchi.
Ilitarajiwa kuwa katika mazingira kama haya, Bunge lingeonyesha mfano. Huu ulikuwa ni wakati wa Bunge kuhakikisha kuwa ripoti hiyo inawekwa hadharani na kujadiliwa kwa kina kama njia ya kulifanya Bunge nalo litoe mchango wake katika vita dhidi ya rushwa.
Kuna watu wameanza tetesi kuwa Spika ameamua kuifunika ripoti hiyo kwa sababu imewasafisha wabunge waliotuhumiwa. Hapa isieleweke kuwa ninawahukumu watuhumiwa kuwa wamekutwa na hatia ya vitendo vya rushwa. Ingekuwa vema ripoti ikatolewa hadharani ili kila mmoja ajue kilichomo na kupunguza tetesi na minongono.
Kama ripoti itakuwa imewasafisha waliotuhumiwa hilo litakuwa ni jambo jema. Ni lazima kutakuwa na ushahidi unaoonyesha ni kwa jinsi gani watuhumiwa hawahusiki na tuhuma hizo. Unataka nini zaidi ya hilo kama lengo lako ni kuhakikisha kuwa Bunge linabaki kuwa chombo kisafi katika uongozi wa nchi?
Lakini kama ripoti inawatia hatiani watuhumiwa hilo nalo ni jambo zuri. Ni nafasi nzuri ya Bunge kuonesha dhamira yake ya dhati ya kupambana na rushwa hata kama inawahusisha wabunge.
Inavyoelekea Bunge limejipanga kwa ajili ya kujikinga lenyewe pale linapotuhumiwa kwa sababu hata sheria zilizopo kuhusiana na mambo yanayofanywa na Bunge nazo zipo kwa mkondo huo huo. Mfano mzuri ni sheria ya Haki, Wajibu na Mamlaka ya Bunge. Kati ya mambo mengine, sheria hii inakataza kwa mtu au taasisi yoyote (naamini waliolengwa kwa kiasi kikubwa ni waandishi wa habari na vyombo vya habari) kuandika taarifa yoyote inayofanyiwa kazi na Bunge au kamati yake.
Mtu au taasisi itakayokiuka sheria hiyo anahesabiwa kuwa ametenda kosa ambalo lina adhabu yake kisheria. Nilimsikia Naibu Spika Job Ndugai hivi karibuni akiikariri sheria hiyo wakati alipowapiga mkwara waandishi wa habari baada ya gazeti moja kuripoti kuhusu ripoti ya kamati ndogo iliyowachunguza wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa.
Kwa mara nyingine nilishangazwa ni kwa nini taasisi kama Bunge inahitaji sheria kali za kuilinda dhidi ya taarifa zake kuwekwa hadharani. Ninaamini kuwa Bunge, kama chombo cha uwakilishi wa wananchi, hakipaswi kuwa na siri nyingi. Bunge ni moja ya taasisi ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa uwazi wa hali ya juu ili wananchi waliowatuma wawakilishi wao wajue kwa kina ni nini hasa wawakilishi hao wanakifanya.
Ukiacha sheria hiyo, pia hata vikao vya kamati siku hizi navyo vimegeuka kuwa siri kubwa. Kwa mfumo wa utendaji kazi wa Bunge, mambo mengi ya maslahi kwa wananchi yanajadiliwa kwenye ngazi za kamati. Inashangaza kuwa waandishi wa habari wanazuiwa kuhudhuria vikao hivyo vya kamati.