Maafisa Watano wa Polisi Wauawa kwa Guruneti Kenya.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Kundi la kigaidi la Al-shabab kutoka nchini Somalia, limewaua maafisa watano wa polisi wa Kenya katika akaunti ya mandera kaskazini mwa nchi hiyo.

Gavana wa kaunti hiyo Ali Roba amesema maafisa hao walishambuliwa baada ya kuviziwa wakiwa ndani ya gari lao katika eneo la Dimu.

Ripoti zinasema afisa mwingine wa polisi ametoweka baada ya shambukizi hilo lililotokea wakati maafisa hao wakisindikiza basi la abiria kwenda mjini mandera.

Gavana Roba amelaani mauaji hayo ya polisi na kusema wakaazi wa kaunti hiyo walikuwa na habari za uwezekano wa kutokea shambulizi hilo na kuzitoa kwa maafisa wa usalama lakini zilipuuzwa.

"Inasikitisha kuwa raia walikuwa na taarifa hizi wakazisambaza alisema"

Hii ni mara ya tatu kwa basi la abiria aina ya makkah kushambuliwa na kundi hilo, likiwa njiani kutoka jijini Nairobi kwenda mjini mandera.

Ripoti za kiinteljensia mwishoni mwa mwezi uliopita, zilieleza kuwa washukiwa 45 wa al-shabab waliingia nchini kenya tarehe 29 kutokea nchini somalia.

Tangu mwaka 2011 jeshi la kenya lilipoingia somalia, nchi hiyo imekuwa ikishambuliwa na magaidi wa al-shabab, ambayo kwa sasa yamepungua hivi karibuni.
2156f3eb63adc0312e9fb0fb799afcb2.jpg
 
Kitu gani kinachowafanya hao wakenya waendelea kuwepo huko Somalia?

Kwa nini wasiwaachie Al Shaabab hiyo nchi yao?
 
Kitu gani kinachowafanya hao wakenya waendelea kuwepo huko Somalia?

Kwa nini wasiwaachie Al Shaabab hiyo nchi yao?
Ni heri jeshi likarudi na kuimarisha mipaka yao kuliko kung'ang'nia Somalia lakini hawasikii hawa viongozi
 
Kitu gani kinachowafanya hao wakenya waendelea kuwepo huko Somalia?

Kwa nini wasiwaachie Al Shaabab hiyo nchi yao?
Yaweza kuwa wako kulinda maslahi ya Kenya like what Russia is doing in Syria or in case Al shabaab watakiwa pale inaweka usalama wa Kenya hatatini...though sijafuatilia kiini na sababu za Kenyans army to be in Somalia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom