Maafisa wa usalama Myanmar wamuua muandamanaji kwa risasi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Vikosi vya usalama vya Myanmar vimemuua kwa kumpiga risasi mwandamanaji mmoja, wakati serikali ya Australia ikithibitisha kuwasaidia raia wake wawili waliokuwa kizuizini kujaribu kuondoka nchini humo.

Watu wawili wamejeruhiwa wakati wa makabiliano ya vikosi vya usalama na waandamanaji. Mamia ya madaktari na wauguzi waliandamana mwishoni mwa Juma katikati mwa Mandalay, mji wa pili kwa ukubwa Myanmar.

Takribani watu 250 wameuwawa tangu kutokea mapinduzi ya Februari na zaidi ya watu 2300 wanashikiliwa.

Myanmar ilitumbukia katika mgogoro tangu wanajeshi walipomuondoa madarakani kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi mwezi uliopita, hatua ambayo ilichochea maandamano ya nchi nzima ya kudai demokrasia.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuwawekea vikwazo maafisa 11 wa kijeshi katika mkutano utakaofanyika kesho Jumatatu.
 
Wao walivyoua watu haikuwa issue ila sasa ndio wameona ukiukwaji

Fardomas fakafuku pambaf kabisa onesheni tu miguvu yenu ila hiyo ni rasha tu mvua itawajia tu siku moja na kibri na jeuri yote vitaisha.
 
Back
Top Bottom