Maafisa mikopo Benki acheni hizi tabia!

Maafisa mikopo Benki acheni hizi tabia!

Kiteitei

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2009
Posts
1,600
Reaction score
1,575
Hivi nyie binadamu mna matatizo gani?

Unapooenda benki kuomba mkopo watakusumbua ile mbaya, mara hiki bado mara kile, ooh twende tukakague dhamana n.k.

Vyote hivyo sina tabu navyo kwani ni taratibu za benki. Muda huu wanakuwa wanakuwekea sura ya mbuzi ila ukishakamilisha wanaanza kujichekelesha.

Mkopo ukitoka tuu wanakutolea macho kama paka aliyeonyeshwa samaki. Kumbe hapo wanataka uwavutie kapasenti kama vile umefanyiwa favour kukupa mkopo!

Utafikiri kwenye rejesho mtasaidiana lakini ukipitisha tu rejesho wanakuchimba mkwara kama mkuu fulani huko kwa wanyamwezi. Dawa ni kuwa mpole ukishafanikiwa unawablock tuu
 
mbona tunafundishwa kuwa "benki hujiendesha kwa 90% kutokana na riba za mikopo huku 10% tu utokana na amana za wateja au hizo ni benki za Ulaya na Marekani?....mibenki hii ikifirisika eti ni kosa la JPM, watanzania IQ zetu ni Mungu tu ndiye anayeweza kuzi-grade!
 
Umetutukana wengi ila fresh tu, tutaonana kwenye marejesho.
 
Ni wapuuzi sana hao jamaa,kazi kuvaa kibishoo halafu njaa kali sana.Kuna moja alikuwa Mwanza(Wilayani) alileta upuuzi kwangu na kwa wananchi wengine innocent kabisa na ilikuwa tabia yake kuomba omba ovyo ili afanikishe mkopo.Nilimripoti head quarter akapigiwa simu akawa anatetemeka.Siku nipo safarini toka dar napigiwa simu nikachukue mkopo,ikawa kila mara wanapiga simu nikachukue mkopo.Niliwaeleza sitaki kwa sababu ya ujinga wa bwana mikopo wao.Head quarter nilimwambia sichukui pia nimemsamehe.Nasikia baada ya miaka 2 au 3 walimfyekelea mbali.Wapuuzi kweli kweli hao.Kama afisa mikopo wa benki ni mwanamke,huwa wana discipline sana ya kutoomba fedha hovyo!!
 
mbona tunafundishwa kuwa "benki hujiendesha kwa 90% kutokana na riba za mikopo huku 10% tu utokana na amana za wateja au hizo ni benki za Ulaya na Marekani?....mibenki hii ikifirisika eti ni kosa la JPM, watanzania IQ zetu ni Mungu tu ndiye anayeweza kuzi-grade!
Labda wewe, sisi watanzania wenye akili timamu, tunajua jpm kaharibu uchumi wa nchi
 
Hiyo mikopo Mara nyingi sana huwafirisi wafanyabiashara bora kupambana na kidogo unachopata kuliko kukopa mikopo yenye riba kubwa mwisho wa siku unafunga duka na kurudisha fremu
 
Hiyo mikopo Mara nyingi sana huwafirisi wafanyabiashara bora kupambana na kidogo unachopata kuliko kukopa mikopo yenye riba kubwa mwisho wa siku unafunga duka na kurudisha fremu
Trump pamoja na kurithi mijimali kutoka kwa baba yake nasikia aliendelea kukopa ili kuwekeza, tatizo langu na wewe tunakopa kununua "assets" na sio "liability". Hapa sizungumzii assets kama Lowassa na Sumaye..
 
Aha a a Ndebile , mhola? Naona umempa majibu konki
 
Back
Top Bottom