Maadhimisho ya siku ya sheria nchini

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,873
8,798
Kuelekea maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambapo maadhimisho hayo yanatarajia kuadhimishwa tarehe 2/2/2017. Mahakama zetu za Tanzania hazina budi kufanya mambo yafuatayo:

1. Mahakama zote zitumie lugha ya kiswahili badala ya kiingereza ktk taratibu za kufungua na kutoa maamuzi, hii itawasaidia wananchi kuelewa kwa wepesi haki zao, wananchi wengi wa kawaida wameshindwa kuelewa au kufuatilia haki zao Kwa sababu ya lugha inayo tumiwa na mahakama za juu kuwa ya kiingereza. Hizi ni Mahakama za watanzania sio taifa jingine tutumie kiswahili ili kujenga dhana ya uwazi na urahisi kwa wanyonge walio wengi
 
Naukumbuka msemo wa "Haki sio tu itendeke bali pia ionekane kutendeka" bila shaka mbele ya wasio wanasheria. Ninachokiona leo "Haki sio tu haionekani kutendeka bali sheria hiyo hiyo inatumika kupindisha haki" kwa baadhi ya kesi. (mimi si mwanasheria)
 
Wakati mahakama ikitumia kiswahili basi ujue Yesu anarudi.

Layman anafikiri lugha ya sheria ni rahisi,ni bongo fleva eeh,ndio maana kuna mawakili.
 
Kwa hiyo masikini asiye na uwezo wa fedha za kumlipa wakiri atafanyaje??

Wanyonge tutakimbilia wapi kama sio mahakamani, hakuna budi vikwazo viondolewa ikiwemo lugha ya kiingereza ili hata asiyefika chuo kikuu ajue kinachoendelea
 
Kwa hiyo masikini asiye na uwezo wa fedha za kumlipa wakiri atafanyaje??

Wanyonge tutakimbilia wapi kama sio mahakamani, hakuna budi vikwazo viondolewa ikiwemo lugha ya kiingereza ili hata asiyefika chuo kikuu ajue kinachoendelea
Uwakili ni kazi za watu.
Ufundi ujenzi ni kazi za watu

Udaktari ni kazi za watu.

Una hela unapata huduma bora. Huna kufwa.
 
Bunge letu linaendesha shughuli zake zote pamoja na kumbukumbu zote kwa lugha ya kiswahili vipi ishindikane kwa huu muhimili wa Mahakama??! Mahakama ni za wazungu au watanzania??
 
Back
Top Bottom