MAADHIMISHO SOKOINE DAY CHUONI SUA

KIBITI BOYZ

Member
Mar 31, 2017
14
32
Habari Tanzania.......
Leo ni kilele cha maadhimisho ya hayati waziri mkuu Edward Moringe Sokoine hapa chuoni SUA, ambapo maadhisho hayo yalianza mnamo tarehe 11 na leo ndo kilele cha siku ya kumbukumbu ya kifo chake hayati Sokoine.
Na mgeni rasmi ni waziri wa kilimo mh. Charles Tizeba .
Madhimisho haya yameambatana na maonyesho mbalimbali kwa wadau wa kada mbalimbali ikiwemo mambo yafanywayo na chuo mfano
-maonyesho ya kitengo cha panya wateguao mabomu na kupima TB
-maonyesho juu ya ufugaji wa samaki
-maonyesho ya carbon mornitoring
-maonyesho juu ya wataalam wa mbegu na mengine mengi
Pia wamewaalika wadau kama
-Suma JKT
-wajasiliamali wadogowadogo hasa waliozao la chuo mfano vijana wanaojiuhisha na kilimo cha uyoga
-watu wa damu salama hivyo kuchangia damu na kupima magonjwa mbalimbali,
Nipende kuwapongeza uongozi wa chuo kwa kuamua kuadhimisha haya kwa kumbukumbu ya shujaa wetu hayati SOKOINE basi nipende kuomba iwe mfano kwa taifa letu kuweza kuwaenzi mashujaa wetu katika mambo yote mema yakuliendeleza taifa letu.
NYOTE MNAKARIBISHWA KATIKA MAADHIMISHO HAYA HAPA CHUONI SUA KATIKA KAMPASI YA MAZIMBU UKUMBI WA FREEDOM SQUARE....MUNGU IBARIKI SUA..MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom