Ma Rais wanaoheshimika Afrika

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
47
Ndugu zangu, ninaomba kujua ma Rais wanaoheshimika sana Afrika (hata kama ni wastaafu); wa kwanza hadi wa mwisho. Wasioheshimka wasiandikwe hapa. Naomba tutoe na sababu za (michango yao au ubunifu wao) kuheshimika kwao na ikibidi CV zao.

Kama huna hoja (uthibitisho wa unayoyasema), usichangie au kuchakachua hapa. Ushabiki hautakiwi.

Nafikiria kuwa, kila mwaka ma Rais hawa tuwape tuzo (au kuomba wapewe tuzo) za heshima hata kama wakiwa wameshazipata tayari. Wa kwanza hadi wa Tatu wapewe wakati wa Mkutano Mkuu wa nchi za Afrika.

Tunaweza kutoa vigezo: mfano (1) Elimu yao (2) Uwezo wa kuongoza na maamuzi yasiyoyumba, (3) Uzalendo na utayari wao wa kusaidia watu wao (4) Hotuba zao, (5) Machapisho yao, (6) Mchango wao kwa Afrika na watu wa nchi zao, nk

Je, vigezo hivi vinafaa? Kama havifai au vinahitaji kurekebishwa, naomba tufanye hivyo kwa NIA NJEMA kwa ajili ya Taifa letu na Afrika yetu. Tunaweza kutumia taarifa hizi kama Role model kupata marais kwenye nchi zetu za Afrika kwa siku za usoni, kama italazimika kufanya hivyo......
 
Hiyo kazi ni ngumu sana! Labda kwenye list ya marehemu waliolala! kila mahali utasikia huyu aliiba hiki, kauwa watu, nk!
 
1.Nelson Mandela (South Africa)
1.Joachim Chisano (Mozambique)
2.Hipefunye Pohamba (Namibia)
3.Habryarimama (Rwanda)
4.Merchiout Ndandaye (Burundi)
5.Julius Nyerere (Danganyika)
6.
7.
8.
9.
10.
 
1.Nelson Mandela (South Africa)
1.Joachim Chisano (Mozambique)
2.Hipefunye Pohamba (Namibia)
3.Habryarimama (Rwanda)
4.Merchiout Ndandaye (Burundi)
5.Julius Nyerere (Danganyika)
6. Sir Serese Khama (Botswana)
7. Festus Mogae (Botswana)
8. KK (Zambia)
9.
10.

wapo wachache sana, na wengi ni wazamani, wa sasa sijuhi
 
Ndugu zangu, ninaomba kujua ma Rais wanaoheshimika sana Afrika (hata kama ni wastaafu); wa kwanza hadi wa mwisho. Wasioheshimka wasiandikwe hapa. Naomba tutoe na sababu za (michango yao au ubunifu wao) kuheshimika kwao na ikibidi CV zao.

Kama huna hoja (uthibitisho wa unayoyasema), usichangie au kuchakachua hapa. Ushabiki hautakiwi.

Nafikiria kuwa, kila mwaka ma Rais hawa tuwape tuzo (au kuomba wapewe tuzo) za heshima hata kama wakiwa wameshazipata tayari. Wa kwanza hadi wa Tatu wapewe wakati wa Mkutano Mkuu wa nchi za Afrika.

Tunaweza kutoa vigezo: mfano (1) Elimu yao (2) Uwezo wa kuongoza na maamuzi yasiyoyumba, (3) Uzalendo na utayari wao wa kusaidia watu wao (4) Hotuba zao, (5) Machapisho yao, (6) Mchango wao kwa Afrika na watu wa nchi zao, nk ....

-Mkuu kwa nikuchallenge kidogo...kama umeamua kuweka hii kitu hapa kubali mawazo ya watu,kusema wasioheshimika wasiwekwe ina maana una vigezo vya hao unaoita wasioheshimika...
-Mbili kigezo cha elimu nilitaka kujua km kinajumuisha na hizi degree za kupeana ama ni elimu ya darasani!
-Uwezo wa kuongoza ni kigezo kizuri ila natamani pia kujua katiba za nchi husika (ambazo hao viongozi bora wametoka) namna zimezingatiwa na jinsi zimegusa maeneo muhimu kijamii!
-Uzalendo na utayari wa kusaidia watu sina neno hapa ila kigezo cha hotuba na machapisho bado inabidi kiangaliwe upya kwa kua hotuba mara nyingi wanaandaliwa!

-Na kwa mtazamo wako inafaa kiongozi kua bora km akikidhi vigezo vitatu ktk vingi ambavyo hukuweka? Ni mtazamo tu,niombe radhi kwa kutojibu swali la msingi!
 
hivi habyarimana mnajua?acheni ushabiki wa kijinga, huyo habyarimana alikua kibaraka wa wafaransa na wabelgiji yeye ndio alio wafundisha wahutu milion 2, kua intarahamwe amco waliofanya genocide ya watusi mwaka 94. Ushabiki bila kua data unaudhi sana.thread imekaa kimajungu na wala sichangii kama kwa elim basi kikwete anaongoza katukiwa phd zaidi ya mbili.
 
1. Muamar Gadafi- uwezo wa kuongea muda mrefu kwa hasira na bila kumstahi mtu.
2.Robert Mugabe-hafagilii wazungu
3.Gbagbo-kama meya wa Arusha anatekeleza methali ya Asiyekubali kushindwa......ni mshindani wa kweli.
 
hivi habyarimana mnajua?acheni ushabiki wa kijinga, huyo habyarimana alikua kibaraka wa wafaransa na wabelgiji yeye ndio alio wafundisha wahutu milion 2, kua intarahamwe amco waliofanya genocide ya watusi mwaka 94. Ushabiki bila kua data unaudhi sana.thread imekaa kimajungu na wala sichangii kama kwa elim basi kikwete anaongoza katukiwa phd zaidi ya mbili.

hapa ni kueleweshana punguza jazba.
Watu wanaweza kuwataja hao maraisi bila kujua upande wao wa pili upo vipi sasa kama wewe umeona habyarimana ana madudu yake unasema tu sio hadi upanick.
 
Back
Top Bottom