Ma-DC wapya kutangazwa Mei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ma-DC wapya kutangazwa Mei

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 15 March 2011 23:33
  [​IMG] Waziri
  Mkuu, Mizengo Pinda

  KITENDAWILI cha wakuu wapya wa wilaya kitateguliwa Mei mwaka huu wakati wilaya na mikoa mipya iliyotangazwa mwaka jana itakapoanza rasmi.Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika hotuba yake ya majumuisho baada ya kumaliza ziara ya siku nane mkoani Kagera.

  Alikuwa akizungumzia umuhimu wa wilaya mpya ya Kyerwa iliyomegwa kutoka Wilaya ya Karagwe.“Nimefurahi wilaya mpya ya Kyerwa hakuna ugomvi wa ujenzi wa makao makuu.Walishakubaliana tangu zamani. Tuombe Mungu kufikia mwezi wa tano, DC wa Kyerwa atakuwa ametangazwa na wilaya zote nchini,” alisema Pinda
  Wilaya mpya ya Rorya, mkoani Mara iliwahi kuwa na malumbano juu ya ujenzi wa makao makuu kiasi cha kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wananchi na viongozi kabla ya Serikali kuingilia kati.Pinda alisema uanzishwaji wa wilaya mpya

  utasogeza huduma zaidi kwa wananchi na kuahidi kuwasiliana na Wizara ya Nishati na Madini ili kutumia maporomoko ya Murongo kuzalisha umeme kwa ajili ya Wilaya ya Kyerwa kama mkakati wa muda mrefu wa kutatua tatizo la umeme.
  Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema mgawanyiko ndani ya chama hicho utaendelea kuwapo ikiwa wagombea walioshindwa wataendelea kutoa zawadi majimboni kwa madai ya kumalizia ahadi zao.
  “Anatoa zawadi kwenye jimbo kama nani? Kama uliahidi zamani pitishia kwenye chama ijadiliwe ndani ya kamati ya siasa. Yaliyopita si ndwele chama kisaidie kurudisha mshikamano,” alisema Pinda.
  Alisema wagombea walioshindwa ndani ya chama hicho na kuendelea kutoa zawadi kama pikipiki na baiskeli kwenye majimbo ni dalili za kutaka kuleta fujo katika maeneo hayo. Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Pinda alisema kuna umuhimu wa Watanzania kutimiza wajibu wao kwa misingi ya kutobaguana.
  Katika majumuisho hayo, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye alimweleza Waziri Mkuu kuwa migogoro ya kisiasa katika himaya yake ni haramu na kuwa wanachama wake wote watapata fursa sawa.
  Mkoa wa Kagera umekuwa wa kwanza kutembelewa na Waziri Mkuu tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Pia hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Pinda kufanya ziara ya kiserikali mkoani hapa akiwa na wadhifa huo.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  twaitaji utekelezaji wenu serikalini, sound zishatuchosha!
   
Loading...