Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, mapema leo amekataa kusomwa na kujibiwa maswali ya wabunge wawili ambao wamechaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Amesema, haiwezekani Mkuu wa Wilaya ambae ni sehemu ya serikali kuihoji serikali hiyo hiyo ambayo yeye ni sehemu yake.
Maoni yangu: Kwanza namsifu Mwenyekiti Mhagama kwa kutambua hilo, kwa sababu amesema kwa kweli hakuna kanuni inayoongelea ni nani anaruhusiwa kuuliza swali bungeni, amesema ana mamlaka ya kuamua kukataa au kukubali swali la mtu yeyote, (hata la Taso wa JamiiForums?!) . Pili ni bahati mbaya sana Rais Kikwete ana hulka ya kulimbikiza vyeo kwa watu ambao wanaishia kuwa kwenye mihimili zaidi ya mmoja. Sasa wewe ni Mbunge na ni mwana serikali, unawajibika kwa bunge kama serikali au unaisimamia Serikali kama mbunge?
Hayo maswali yaliyokataliwa, ina maana duku duku za wananchi zilizobebwa na maswali hayo hayataweza kupatiwa msaada au majibu, hivyo wananchi wamekosa uwakilishi kwa namna moja ama nyingine. Lini tunakuwa na utengano kamili wa mihimili ya nchi?